dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 3, 2015

Balozi wa Msumbiji Afika Ikulu Kumuaga Dk. Shein leo

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe,Vicente Mebunia Veloso alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe,Vicente Mebunia Veloso alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe,Vicente Mebunia Veloso baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,([Picha na Ikulu.]

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                                           3.8.2015
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Msumbiji na Tanzania ni nchi zenye historia katika uhusiano na ushirikiano wao hivyo kuna kila sababu ya kuendelezwa na kuimarishwa kwa manufaa ya pande mbili hizo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaemaliza muda wake wa kazi hapa nchini Mhe. Vicent Mebunia Veloso, yaliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kuaga.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbuji ni wa kihistoria hivyo hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika mashirikiano katika sekta kadhaa za maendeleo ni muhimu na zinamsingi kwa nchi zote mbili.

Dk.Shein alisema kuwa Tanzania ikiwemo Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na Msumbiji ambao umepelekea wananchi wake kuishi kama ndugu kwa miaka mingi sambamba na juhudi zinazochukuliwa na serikali za nchi hizo katika kuendeleza hatua hiyo.Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Msumbiji na kueleza kuwa mashirikiano yanayoendelezwa yatasaidia katika uimarishwaji wa sekta za maendeleo zikiwemo elimu, kilimo, gesi na mafuta, utalii na nyenginezo.

Akizungumzia kwa upande wa sekta ya elimu, Dk. Shen alisema kuwa hatua za ushirikiano uliopo hivi sasa katika sekta hiyo kati ya Msumbiji na Tanzania umeweza kuleta mafanikio mazuri na kusisitiza haja ya kuendelezwa kwa upande wa Zanzibar kupitia SUZA kwani tayari chuo hicho kinafundisha lugha kadhaa ikiwemo Kiswahili, Kireno,Kichina,

Dk. Shein alimpongeza balozi huyo kwa mashirikiano mazuri aliyoyatoa katika muda wake wote aliofanya kazi hapa nchini sambamba na kueleza kuwa ujio wa Rais Filipe Nyusi hivi karibuni hapa nchini umeonesha wazi uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Msumbuji pamoja na kuweko kwa makubaliano kadhaa ambayo yataimarisha uhusiano huo.

Nae Balozi wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Vicent Mebunia Veloso alitoa pongezi kwa wananchi na viongozi wa Tanzania kwa kumpa mashirikiano mazuri wakati akiwa nchini akitekeleza majukumu yake ya Ubalozi wa nchi yake.

Balozi Veloso alisema kuwa Msumbiji inajivunia uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ambao ni wa muda mrefu hali ambayo imepelekea kuwepo kwa makubaliano kadhaa katika sekta za maendeleo ambayo baadhi yake yameshaanza kutekelezwa na kufanyiwa kazi.

Katika maelezoa yake Balozi huyo wa Msumbiji alisema kuwa  makubaliano yaliofikiwa katika ujio wa Rais Filipe Nyusi pamoja na yale aliyoyarisi kutoka kwa Rais aliemaliza muda wake Mhe. Armando Guebuza pamoja na viongozi wa Tanzania yanaweza kuimarisha zaidi uhusiano wa kimaendeleo kwa nchi mbili hizo.

Aidha, Balozi huiyo alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa nchi yake itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo ambao unahistoria na hivi sasa tayari matunda yake yanaonekana hasa katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.

Katika mazungumzo yao viongozi hao pia, waligusia haja ya kukuza uhusiano na ushirikiano katika sekta ya usafiri na usafirishaji hatua ambayo itarahisisha safari za anga na bahari kati ya Msumbuji na Zanzibar.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments :

Post a Comment