Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 29, 2015

Dk Shein aishukuru China sekta ya afya

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kujengwa upya kwa hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba kutawezesha hospitali hiyo kuwa ya kisasa na inayokidhi viwango vya kimataifa.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo jana, Dk. Shein, aliishukuru serikali na wananchi wa Jamhuri ya watu wa China kwa msaada wao mkubwa katika kuimarisha sekta ya afya nchini ikiwemo ujenzi wa hospitali hiyo.
“Hawa (wachina) ni marafiki zetu wa kweli kwani akuufaaye kwa dhiki ndie rafiki” Dk. Shein aliwaeleza wananchi wa mji wa Mkoani na viongozi wa serikali waliohudhuria hafla hiyo.
Alitoa shukrani maalum kwa Rais Xi Jing Ping kwa kuendeleza udugu na urafiki kati ya watu wa Zanzibar na China kwa kufuata nyazo za viongozi waliomtangulia hayati Mao Dze Tung na Cho en Lai ambao walioasisi urafiki huo na viongozi wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Nyerere na Marehemu Abeid Amani Karume.
Alisema ni jambo la fahari kuona kuwa urafiki wa nchi hizo umekuwa wa mafanikio makubwa na kutoa mfano wa mchango wa serikali na wananchi wa nchi hizo mbili mara baada ya Mapinduzi hadi leo.
Alisema alipoomba msaada kwa viongozi wa China kuhusu kujengwa hospitali hiyo alifanya hivyo kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 ibara152 ambayo ilielekeza kuendeleza kuimarisha sekta ya afya ikiwemo kuifanya hospitali ya Abdalla Mzee kuwa hospitali ya mkoa.
Kuhusu ubora wa hospitali hiyo alieleza kuwa imezingatia vigezo vyote vya hospitali za kisasa na kwamba itakuwa na vifaa vyote vya kisasa vya uchunguzi wa maradhi ambavyo vitatolewa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaweka kifaa kipya cha uchunguzi wa maradhi kijulikanacho kama Magnetic Resonance Imaging (MRI).
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment