WAPIGA MAKACHU maarafu wa Forodhani, kutoka mjini Zanzibar, wamempongeza bi Arafat Ibrahim Mustafa kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jumuiya ya Diaspora ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada, ijulikanayo kama ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association).
Wapiga makachu hao pia wamempongeza Bw. Donald Trump kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa 47 wa Marekani.
Pongezi hizo walizitoa wapiga makachu hao walipokuwa wakipiga makachu Forodhani mjini Zanzibar, kama inavyoonekana kwenye video zao za hapa chini.
Tarehe 26 October, 2024, Bi Arafat alichaguliwa na Board of Directors (BoD) wa Jumuiya ya Zacadia kuchukuwa nafasi ya urais wa Jumuiya hii baada ya Rais wa zamani Shk Omar Ali Said kuachia ngazi kutokana na sababu zake binafsi.
Bi Arafat ni mmoja ya waanzilishi wa Jumuiya ya Zacadia katika mwaka 2011.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais bi Arafat alikuwa Chief Secretary wa Jumuiya hii na kabla ya hapo alikuwa Manager wa Management team.
Bi Arafat anayo digrii ya pili (Masters) katika fani ya Community Services & Social Welfare na ni muhitimu wa somo la political science kutoka chuo cha diplomatsia cha Dar Es Salaam, Tanzania.
Bwana Donald John Trump ni mfanyabiashara, mjasiriamali wa Marekani aliyezaliwa tarehe 14 Juni 1946, Queens, New York. Alikuwa Rais wa 45 wa Marekani kutoka Januari 20, 2017 hadi Januari 20, 2021. Bw. Trump ni maarufu kama mfanyabiashara wa mali isiyohamishika, akiwa na kampuni ya Trump Organization ambayo inajulikana kwa kujenga majengo maarufu na hoteli duniani kote.
Kabla ya kuingia kwenye siasa, Bw. Trump alijulikana kama mmiliki wa kasino, hoteli, na miradi ya kifahari, na pia alikuwa mwenyeji wa kipindi cha televisheni cha The Apprentice.
Katika kipindi chake cha urais, Bw. Trump alikumbana na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kuingilia kati kwa Urusi katika uchaguzi wa 2016. Alikosa kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa 2020 aliposhindwa na Rais wa sasa Rais Joe Biden. Katika uchaguzi wa 2024, Bwana Donald Trump alishinda na tarehe 20 January, 2025 ataapishwa kwa mara yapili kama Rais wa 47 wa Marekani.
No comments :
Post a Comment