Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 29, 2015

Ukawa kufunika

  Lowassa kuibua mazito

  Kujibu mapigo leo
Sehemu ya Jukwaa litakalotumiwa na Chadema katika uzinduzi wa kampeni za urais zinazotarajiwa kuzinduliwa katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo. PICHA:SELEMANI MPOCHI
Hatimaye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anatarajiwa kuzindua kampeni zake leo kwenye Viwanja vya Jangwani.
 
Katika uzinduzi huo Chadema kimewataka Watanzania na wananchi wanaotaka mabadiliko kujitokeza kwa wingi na kumsikiliza mgombea wao akitangaza mikakati ya ushindi. 
 
Mratibu wa uzinduzi wa kampeni hizo, Deogratias Munishi, akizungumza na waandishi wa habari jana katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam,  alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa asilimia 90.
 
Uzinduzi huo unafanyika baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuruhusu viwanja hivyo kutumiwa cha chama hicho baada ya kuwepo kwa utata wa kuzuiwa.Chama hicho ambacho kilipanga kufanya uzinduzi wake Agosti 22, katika Uwanja Mkuu wa Taifa, kilishindwa baada ya serikali kuzuia kutumiwa kwa matumizi ya kampeni kwa vyama vyote vya siasa.
 
WAGENI NCHI MBALIMBALI KUHUDHURIA
 
Munishi alisema katika uzinduzi huo viongozi na wanachama mbalimbali kutoka katika matawi ya Chadema  nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria pamoja na viongozi wote wa Ukawa. 
 
"Tunatarajia kuwa na wageni kutoka nchi ambazo tunawawakilishi wetu,  pia tunatarajia kupokea viongozi na wanachama kutoka mikoa mbalimbali ikiwamo Arusha, Morogoro na Pwani, "alisema.
 
Aliwahimiza wananchi wanaoishi jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za chama na mikakati ya mgombea wa chama hicho atakayoifanya endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
UMEME TANESCO
Aidha,  alidai kuwa kama Shirika la Umeme nchini  (Tanesco) linakusudia kukata umeme siku hiyo, haliwezi kuzuia wananchi kuzifahamu sera zilizoandaliwa na Ukawa kwa kuwa watazunguka nchi nzima kuzitangaza.
 
"Kama Tanesco wanakata umeme hawataweza kuzuia wananchi kusikia sera nzuri zilizoandaliwa na wagombea wetu kwani tutapita nchi nzima na tukimaliza uzinduzi ziara ya mikoani zinaanza kesho, "alisema Munishi.
 
 KUANZA ZIARA IRINGA
Akizungumzia ratiba za Mgombea wao wa urais na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, alisema wataanza mikoa ya Iringa na Mtwara.
 
Munishi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,  alisema Lowassa ataanzia mkoa wa Iringa kwa kufanya  mikutano minne.
 
"Baada ya kesho (leo), Lowassa keshokutwa (kesho) atakuwa Iringa katika maeneo manne ya Mufindi, Kilolo, Kalenga na baadae jioni atafanya mkutano mkubwa wa hadhara Iringa mjini,"alisema.
Alieleza kuwa,  Mgombea Mwenza, Duni Haji atakuwa mkoani Mtwara katika maeneo manne ambayo ni Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na baadae Mtwara mjini ambako atafanya mkutano mkubwa wa hadhara jioni.
 
WAJIPANGA KULINDA RAIA
Mbali na Maandalizi hayo, Munishi alisema wamejipanga kulinda wananchi wote watakaojitokeza kushiriki uzinduzi huo pamoja na mali zao.
 
Alisema polisi wanataarifa za mkutano  wa leo, isipokuwa ni wajibu wao pia kuhakikisha ulinzi na Usalama unakuwepo.
 
USAFIRI WA ANGA
kwa upande wake,  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano,  Tumaini Makene,  alisema watatumia usafiri waliopanga kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na nchi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment