dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 9, 2015

A clarion call to all Tanzanians to vote for Lowassa


Wandugu, nia yetu sio kumchagua mtu anaesema kuwa anaichukia rushwa au atajenga viwanda katika kila kijiji. Kuichukia rushwa peke yake wakati KATIBA ya nchi inalinda rushwa ni wendawazimu mtupu.

Tunachotaka ni KATIBA yenye maana na sio inayowahifadhi watu fulani madarakani au chama fulani. Tukiipata Katiba tuitakayo wengi basi rushwa itapotea wenyewe.

Itakuwa inamaana gani kumpata Rais anaeichukia rushwa lakini anataka kutuletea Katiba ile ile mbovu inayopendekezwa?

Itakuwa kunamaana gani kutujengea viwanda katika kila kijiji wakati Katiba ya nchi ni mbovu na inawalinda wachache tu ili waendelee kututawala?

Kama unataka usiipoteze kura yako, please, usinisikilize mimi bali kaa chini chumbani kwako peke yako na ufikirie baina ya Magufuli na Lowassa nani unafikiria kwa akili yako iliyotulia atatuletea Katiba ambayo sote tunaitaka?

Hivyo Magufuli kawahi hata katika mkutano wake mmoja kutamka kuwa atabadilisha chochote katika Katiba Inayopendekezwa? Hivyo Katiba Inayopendekezwa ndio Katiba tunayoitaka Watanzania?

Please, leave aside porojo za Richmond. Richmond sote tunajua kuwa ilikuwa project ya nani. Lowassa peke yake asingeliweza kufanya kitu bila ya kuungwa mkono.

Tafadhalini Watanzania, tusiwe wapumbavu na malofa. Tumchaguwe Lowassa ili tuipate Katiba tuitakayo, ili tuudumishe na tuuimarishe Muungano wetu na udugu wetu wa damu, ili watolewe waliowekwa vizuwizini bila ya makosa. Yote haya yatawezekana, mpe kura yako Lowassa tarehe 25 October, 2015!


No comments :

Post a Comment