dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 22, 2015

Askofu Mkude: Uchaguzi wa mwaka huu mgumu.

Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphoy Mkude.
Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphoy Mkude, amesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaofanyika Jumapili ni mgumu kuliko wa miaka iliyopita, hivyo endapo haki haikutendeka kuna, hatari ya kupotea kwa amani.
Askofu Mkude alitoa kauli hiyo mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi huo.
Alisema ugumu wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unatokana na baadhi ya viongozi wa chama kimojawapo kutoa kauli za kuashiria kuwa ni lazima washinde ikibidi hata kwa bao la mkono, kauli ambayo alieleza zinaashiria nia mbaya, huku viongozi wakuu wa chama hicho wakishindwa kukemea.
Askofu Mkude alisema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya mfumo wa vyama vingi, hivyo ni vyema wananchi wakapewa nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka bila kujali itikadi, rangi, ukabila wala udini kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliopangwa.
Alisema si jambo jema kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa kutoa kauli za kulazimisha kushinda katika uchaguzi huo hata kama pale wananchi wanapokataa hali ambayo inaweza kuchochea kuvurugika kwa amani.
Askofu Mkude aliwataka viongozi na wagombea kuacha kauli za uchochezi  ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika uchaguzi huo na badala yake wasisitize amani.
Alisema viongozi wanapaswa kuyakemea makundi ya vijana badala ya kuyachochea uvunjifu wa amani  na kuyatumia katika kampeni mbalimbali ili uchaguzi ufanyike kwa utulivu na amani.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment