Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 26, 2015

Baadhi ya waangalizi kimataifa waeleza waliyoyaona vituoni!

Mgombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee.
Baadhi ya waangalizi wa kimataifa waliokuwa wakifuatilia upigaji kura katika vituo mbalimbali jana, wameeleza kuridhishwa na hali ilivyokuwa, pamoja na kuwapo kwa kasoro ndogondogo. 
 
Mwangalizi wa uchaguzi wa kimataifa, kutoka ubalozi wa Ubelgiji nchini, Paul Cartie, alisema upigaji kura ulienda vizuri japo katika baadhi ya maeneo ulifanyika kwa taratibu sana.
 
Alisema katika baadhi ya vituo alivyotembelea alishuhudia mtu mmoja akitumia hadi dakika 10 kupiga kura na kuwafanya watu wengine kusubiri zamu zao kwa muda mrefu.
 
Alisema amefurahishwa na mwamko mkubwa ulioonyeshwa wa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
 
Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Osterbay, jijini Dar es Salaam, Muangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Judith Sargentini, alisema wametembelea vituo 400 mijini na vijijini na kwamba katika maeneo hayo yote wameshuhudia uchaguzi umeenda vizuri licha ya kuwapo kwa changamoto ndogondogo.Hata hivyo, alisema ripoti kamili kuhusiana na uchaguzi wanatarajia kuitoa leo.
 
Kwa upande wake, Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Madola, Rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan, alisema hazungumzii lolote mpaka leo watakapotoa ripoti yao.
 
JIMBO LA KAWE
Mgombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee, alisema katika kituo cha Makongo Juu alikopigia kura,  kulikuwa na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa vifaa.
 
Naye mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, ambaye alipiga kura katika kituo cha Ununio, alilalamikia makarani wanaoandikisha wapiga kura kuendesha kazi hiyo taratibu.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment