dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 20, 2015

CUF yafunga kampeni zake za majimbo leo viwanja vya Malindi!

   Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Malindi Mjini Zanzibar.
 Wafuasi na wapenzi wa CUF wakifuatilia mkutano huo wa mwishi wa kampeni za majimbo katika viwanja vya Malindi mjini Zanzibar.
 Wafuasi na wapenzi wa CUF wakifuatilia mkutano huo wa mwishi wa kampeni za majimbo katika viwanja vya Malindi mjini Zanzibar.
 Wafuasi na wapenzi wa CUF wakifuatilia mkutano huo wa mwishi wa kampeni za majimbo katika viwanja vya Malindi mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimtambulisha mgombea Ubunge wa Jimbo la Malindi Bw. Ali Saleh Alberto katika viwanja vya Malindi Mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad (OMKR)

Chama Cha Wananchi CUF kimefunga rasmi kampeni zake za majimbo, na kuwataka wanachama kujiandaa kwa ajili ya upigaji kura ifikapo tarehe 25 mwezi huu.

Akizungumza katika mkutano wa mwisho wa kampeni za  majimbo uliofanyika viwanja vya Malindi kwa ajili ya majimbo ya Kikwajuni na Malindi, Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais, itaongeza nafasi za ajira na maslahi ya wafanyakazi, na wala sio kuwafukuza wafanyakazi kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema lengo lake ni kuimarisha utendaji wa wafanyakazi wakiwemo wa vikosi vya SMZ, na kupanga kukibadilisha jina Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo KMKM kuwa kikosi cha walinzi wa baharini (Coastal Guards).Nae Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, ameiomba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuweka mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi wa haki na amani.

Amesema Tume hiyo inaweza kuandaa uchaguzi usio na mizengwe, na kwamba kufanya hivyo kutaonesha ukomavu wa demokrasia na kuijengea sifa Zanzibar katika ulingo wa siasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu, amelipongeza jeshi la polisi kwa ushirikiano unaotoa kwa vyama vya siasi katika kipindi hiki cha kampeni katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

Amesema Chama Cha CUF kitaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo, ili kuona kuwa kampeni za uchaguzi zinamalizika salama bila ya kuwepo mivutano katika ya polisi na wananchi.

Chama hicho kimepanga kufunga rasmi kampeni zake za uchaguzi tarehe 20 mwezi huu kwa upande wa Pemba na tarehe 22 kwa upande wa Unguja, ili kutoa fursa kwa wanachama kujiandaa kupiga kura. 

No comments :

Post a Comment