dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 20, 2015

Shein: Zanzibar itakuwa kama Dubai!

Image result for dubai highrise images
Dubai
Image result for dubai highrise images

Image result for dubai highrise images
Burj Khalifa of Dubai.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein 
Zanzibar. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein amesema akichaguliwa atavifanya visiwa hivyo kuwa mji wa kisasa wenye hoteli za nyota tano, viwanda na uwanja wa kimataifa wa mpira.
Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye mkutano wake wa 25 wa kampeni za uchaguzi uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk Shein alisema Zanzibar itafanana na miji mikubwa duniani kama Dubai.
Alisema tayari kuna eneo maalumu kwa ajili ya ujenzi huo ambalo limeshatengwa katika eneo la Fumba na kwamba kiwanda cha kisasa za kuzalisha maziwa cha Azam kimeshaanza kazi.
Alisema katika eneo hilo, pia utajengwa uwanja wa mpira wa kimataifa utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watu 45,000.
“Mji wa Fumba utakuwa eneo huru la uwekezaji, yatajengwa majengo yenye zaidi ya ghorofa 20 kwa ajili ya makazi na wanaofanya kazi hii ni wawekezaji kwa kushirikiana na Serikali.
“Mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Wazanzibari, wasikudanganyeni wapinzani kwa ahadi hewa, ninachokisema ni mipango ya Serikali inatolewa na rais wengine waongo,” alisema.
Alisema Serikali inaingia makubaliano kampuni mbalimbali nchi kuhusiana na miradi hiyo akawataka wananchi wamchague ili aiendeleze.
Akiuzungumzia Mji Mkongwe, alisema Serikali itaendelea kuwatumia wawekezaji kwa ajili ya kuyafanyia ukarabati majengo ya Mji Mkongwe ili yaweze kuendeleza historia na kuingizia mapato kupitia utalii.
“Tutalinda historia ya Zanzibar kwa kuboresha majengo ya Mji Mkongwe bila kuathiri mwonekano wake ili kuboresha sekta ya utalii,” alisema.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi alisema maendeleo yaliyopatikana Zanzibar yameletwa na CCM hivyo akawataka wananchi kukichagua chama hicho ili kuendeleza mambo yaliyobaki. Kwa upande wake, Katibu wa Oganaizesheni ya CCM Taifa, Dk Mohamed Seif Khatib aliwataka wananchi waipe kura CCM ili iweze kudumisha Muungano.
Alisema kamwe Wazanzibar wasifanye uchaguzi huu kwa majaribio, bali wakichague chama chenye rekodi ya kudumisha amani na mshikamano.

No comments :

Post a Comment