Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 6, 2015

Dk Magufuli: Ningemuombea kura Dk Slaa kama angegombea ubunge!

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi katika moja ya milutano ya kampeni ya chama hicho. Picha na Maktaba
By Waandishi Wetu, Mwananchi
Karatu. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli jana aliwahutubia mamia ya wakazi wa Karatu na kummwagia sifa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa ni kiongozi mwadilifu na kuongeza kuwa kama angekuwa anagombea katika jimbo hilo, angemwombea kura kwani ni mtu safi bila kujali chama chake.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mbowe mjini Karatu, Dk Magufuli alisema Dk Slaa ni kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa mwadilifu akitetea masilahi ya umma.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu wa Karatu, Dk Magufuli aliwataka kumuunga mkono Dk Slaa kwa uamuzi ambao amechukua.
Dk Slaa, alitangaza hivi karibuni kuachana na siasa za vyama na kujitoa Chadema baada ya kutoridhishwa na kujiunga kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika chama hicho.

No comments :

Post a Comment