dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 23, 2015

Haki, amani vitawale upigaji kura Jumapili.

NA EDITOR

23rd October 2015.

Katuni.
Tangu Agosti 22 mwaka huu kipenga cha kampeni za uchaguzi mkuu kilipopulizwa hadi leo hii siku moja kabla ya muda wa kampeni kumalizika rasmi, Watanzania wamethibitisha kwa vitendo halisi kwamba inawezekana kufanya kampeni za ushindani mkali wa kisiasa bila vurugu.
Watanzania watakumbuka kwamba tangu kuanza kwa kampeni hizi wapo waliokuwa wanabashiri kwamba mwaka huu taifa hili lingeingia machafuko, kisa kampeni za uchaguzi mkuu kwa kuwa tu mwaka huu ushindani wa kisiasa umekuwa wa kiwango cha juu kabisa; tunafarijika kuwa kampeni zinamalizika taifa likiwa imara huku amani na utulivu vikitamalaki.
Tunajua kwamba kwa miaka mingi wapo watu walijitahidi sana kujenga dhana potofu kwamba nchi hii haiwezekani kufanyika kwa maandamano ya amani na hata mikutano ya kampeni ya amani, kwa sababu za kutaka kudhoofisha ukuaji wa demokrasia nchini, hao walivishinikiza vyombo vya ulinzi na usalama kutumia mabavu yasiyokuwa na ulazima wowote kuvuruga shughuli halali za kisiasa. 
Mwaka huu historia mpya imejengwa, kwamba inawezekana kabisa shughuli zenye joto kali la kisiasa zikaendeshwa kwa amani na utulivu; kwamba vyombo vya usalama kwa maana ya Jeshi la Polisi likatimiza wajibu wake wa kulinda mikutano hiyo ili kila mwenye kutaka kuhudhuria, kusikiliza na kuzungumza afanye hivyo bila kubughudhiwa.
Uchaguzi wa mwaka huu ni wa tano kufanyika tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, unaweza kutajwa kuwa ni wa kihistoria zaidi kutokana na ushindani mkali uliopo baina vyama na wagombea wa ngazi ya urais, ubunge na udiwani.
Pamoja na ushindani huu, tunapata faraja kwamba mambo yanaenda sawa. Kwamba pamoja na faida kubwa za maendeleo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano (Tehama), wingi wa simu za mikononi kiasi cha milioni 25 na mitandao ya inteneti ambazo zimerahisisha sana mawasiliano, bado joto la uchaguzi halijaondoa Watanzania kwenye hulka yao ya ustaarabu.
Tunajua uchaguzi ni mchakato, pamoja na changamoto zilizoanza na kazi ya kuandikisha wapigakura idadi kubwa ya wananchi wameandikishwa, kuna wapigakura zaidi ya milioni 22; tumeshuhudia pia ugawaji wa majimbo mpya ya uchaguzi; tumeshuhudia kampeni za ushindani mkali zikienedelea na sasa zinakaribia kabisa ukingoni ili sasa hatua nyingine mbili muhimu zifanyike, yaani upigaji kura, uhesabuji kura na utangazaji matokeo.
Hatua hizi mbili za mwisho, upigaji kura, uhesabuji kura na utangazaji matokeo, ndio nyeti na tete kuliko nyingine zote. Ndizo zinatoa mshindi na aliyeshindwa. 
Tungependa kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikikataa kutumika kisiasa kuharibu uchaguzi huu, kadhalika tungependa kuona Nec na Zec wakitimiza wajibu wao wa kisheria na kikanuni kuhakikisha kwamba kila mgombea anatendewa haki. Anayeshinda kweli ndiye anayetangazwa na kuapishwa.
Ni imani yetu kwamba kama Nec na Zec watatimiza wajibu wao wa kuendesha na kusimamia uchaguzi huu kwa misingi ya sheria na kanuni.
Ni kwa msingi huo tunawataka wagombea wote kuyakubali matokeo ya aina yoyote ama iwe ni kwa kushindwa au kushinda ilimradi tu, mazingira ya upigaji kura, uhesabuji kura na utangazaji wa matokeo yataakisi haki na uhuru wa wapigakura kutumia fursa hiyo kuwachagua wanaowataka kuwa viongozi wao kwa kipindi cha miaka miatano ijayo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment