dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 23, 2015

Huyu ndiye anayeruhusiwa kupiga kura siku ya uchaguzi


By Julius Mathias, Mwananchi
Dar es Salaam. Hayawi hayawi…sasa yamekuwa. Siku ya Watanzania kupiga kura kwa ajili ya kumchagua rais, wabunge na madiwani ni keshokutwa.
Wote waliojiandikisha kwa ajili ya kushiriki tukio hilo la kihistoria, watatakiwa kufika kwenye vituo walikojiandikisha na kupiga kura zao.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 na kufungwa saa 10:00 jioni.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya maandalizi ya muda mrefu, ikiwamo kampeni za wagombea hao zilizofanyika kwa kipindi cha siku 64 nchi nzima zitakazomalizika kesho.
Katika kipindi hicho, wagombea hao walishindana kuwashawishi wapigakura kwa kunadi sera zao na kutoa ahadi mbalimbali watakazozitekeleza endapo watachaguliwa kuingia madarakani.
Sasa Watanzania wako tayari kuisimika Serikali ya Awamu ya Tano kwa demokrasia huru na haki.
Lakini, watakaoruhusiwa kushiriki uchaguzi huo kwa kupigakura ni wale tu wenye sifa na waliofanikiwa kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Mfumo wa Biometric Voters’ Registration System (BVR).
Hawa wasikae majumbani
Ili kufanikisha shughuli hiyo, watu wote wenye sifa zifuatazo wanatakiwa kujitokeza vituoni na kupiga kura. Sifa hizo ni pamoja na raia yoyote wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 na ameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na ana kadi ya kupigia kura, iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mkazi wa kawaida wa eneo analotaka kupiga kura.
Jina lake limeorodheshwa katika daftari la kudumu la wapiga kura au orodha inayobandikwa katika kituo cha kupigia kura.

No comments :

Post a Comment