dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 21, 2015

JK azindua mradi mkubwa wa kusaga kokoto wa bilioni 5.6/- .

Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete, amezindua mradi mkubwa wa kusaga kokoto katika kijiji cha Pongwe-Msungura, kilicho eneo la Msata Wilaya Bagamoyo mkoani Pwani wenye thamani ya Sh. bilioni 5.6.
 
Mradi huo unamilikiwa kwa ubia kati ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la uzalishaji mali (SumaJKT) na kampuni ya Anitasfalt ya Uturuki. Akizungumza wakazi wa uzinduzi huo, Rais Kikwete aliliagiza jeshi hilo kupitia kampuni inayoendesha mradi huo ya SumaJKT Anit Asfalt Co. Ltd, kuona uwezekano wa kuwekeza kwenye teknolojia ya utunzaji mazingira ili kudhibiti vumbi litakalotokana na uzalishaji wa kokoto kuathiri afya ya wanakijiji walio jirani na mradi.
 
“Hatua hii inaweza kuwa mbadala ya wakazi wengine jirani na mradi kushawishika kutaka walipwe fidia ili wahame kwa ajili ya kukimbia vumbi,” alisema.Aidha, Rais Kikwete alimuelekeza Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga, kuona kama kuna tatizo la fidia kwa wakazi waliohama kupisha mradi na kulishugulikia. Naye Meja Jenerali Muhuga,      alisema      mradi huo umeanza baada ya kufarijika kwa  mazungumzo  ya kibiashara na nyaraka za makubaliano kuwekwa saini Desemba 21, mwaka 2010.
 
“Afande Amir Jeshi Mkuu , mtaji wa mradi ni Sh. bilioni 5.6, na SumaJKT inamiliki asilimia 30 sawa na Sh. bilioni 1.68, wakati Anit Asfalt wanamiliki asilimia 70, sawa na Sh. bilioni 3.92,” alisema.
 
Aidha, alisema tayari JKT imelipa fidia ya Sh. milioni 136 kwa wakazi 142 wanaoishi karibu na eneo la mradi kwa lengo la kuwahamisha.
 
Alisema wakazi 138 kati ya 142, tayari wamechukua fidia zao wakati familia nne hazijachukua kutokana na migogoro kati yao .
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment