Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 25, 2015

‘Mchuano CCM, Chadema hautabiriki’-Sungusia


Mkurugenzi wa Utetezi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia
MONDAY, OCTOBER 26, 2015
By Sauli Giliard/Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Mkurugenzi wa Utetezi  wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia amesema matokeo ya awali ya wagombea nafasi ya urais kupitia CCM na Chadema yanadhihirisha kuwa demokrasia ya nchi sasa imekomaa.
Akifanya uchambuzi wa mwenendo wa uchaguzi mkuu kupitia kituo cha luninga cha ITV, jijini Dar mapema leo, Sungusia amesema tofauti na miaka iliyopita, ni vigumu kutabiri chama kitakachoibuka na ushindi hivyo kutoa hamasa ya kufuatilia kinyang’anyiro hicho hadi mwisho.
Hata hivyo, mwanaharakati huyo wa haki za binadamu ametabiri kuwa Tanzania itabadilika kimaendeleo kwani atakayeibuka mshindi atakuwa na changamoto ya kuhakikisha anabadilisha mambo.
“Yeyote atakayeshinda inamlazimu afanye kazi ya ziada ili aweze kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka 2020,” amesema Sungusia.
Hata hivyo, amelitaka Jeshi la Polisi kutowakandamiza watu wataokaoshangilia ushindi kwa kuwa ni kinyume cha haki za binadamu kwa kuwa furaha ni kitu ambacho hakizuiliki kama ambavyo ilivyo kwa mtu anayelia.
Ameongeza kuwa kuwapiga mabomu watu bila sababu ya msingi ni kutengeneza kizazi sugu na kulitaka jeshi hilo kutoleta ubaguzi wakati wa kutekeleza amri ama sheria.

No comments :

Post a Comment