dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 21, 2015

Mwananchi haihusiki na uhuni huu!







Bakari Machumu-Mhariri Mtendaji Mkuu

 
Bakari Machumu-Mhariri Mtendaji Mkuu   
By Bakari Machumu-Mhariri Mtendaji Mkuu
KAMPUNI ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inalaani uhuni ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu ya kutengeneza gazeti feki kwenye mitandao ya kijamii.
Jana, katika mitandao mbalimbali ya kijamii kulikuwa na gazeti mfano wa Mwananchi ambalo lilikuwa likionyesha habari inayowatuhumu viongozi wa Ukawa.
Hii ni mara ya pili kwa kitendo cha watu hao kutengeneza gazeti feki la Mwananchi kwenye mitandao ya kijamii, kwani mwezi uliopita walifanya hivyo pia wakiwa na lengo hilo hilo la kuwasingizia viongozi wa Ukawa.
Kama tulivyotoa angalizo mwezi uliopita, Mwananchi hatuhusiki kwa vyovyote vile na vitendo hivyo vya kihuni na tunaomba wasomaji wetu wawe makini hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu.
-Mhariri Mtendaji Mkuu

No comments :

Post a Comment