dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 6, 2015

NEC kuanzisha kitengo maalum kuhakiki taarifa za wapigakura!

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Mpigakura wa NEC, Giveness Aswile
By Julius Mathias, Mwananchi
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inatarajia kuzindua dawati la huduma kwa wateja ambapo wananchi watatumia kuthibitisha kumbukumbu zao baada ya zoezi la uhakiki wa taarifa kutofanyika kwa watu wengi.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Mpiga kura wa NEC, Giveness Aswile amesema hay oleo alipotembelea ofisi za gazeti hili na kuzungumza na wahariri kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadiliana namna ya kushughulikia changamoto mbalimbali zinazojitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ili kuwatoa hofu wananchi juu ya kukosa ushiriki wa kuchagua mgombea kwa nafasi za urais, ubunge na udiwani, Aswile alisema tume imeona haja ya kuweka kitengo maalumu kitakachotatua kero zinazojitokeza kuhusiana na upigaji kura.
“Taratibu za uanzishaji wa dawati hilo unaendelea na unatarajia kukamilika muda wowote kabla ya kuanza kutoa huduma stahiki. Litahudumia wale wote walioshindwa kuhakiki na kuhamisha taarifa zao wakati daftari lilipopelekwa kwenye maeneo yao kati ya Agosti mpaka Septemba,” alisema Aswile.

No comments :

Post a Comment