dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

Tacceo yaibua dosari 1,000 za kampeni

Mwenyekiti wa Tacceo, Martina Kabisama
By Pamela Chilongola, Mwananchi
Dar es Salaam. Mtandao wa Asasi za Kiraia wa Kuangalia Uchaguzi Tanzania (Tacceo), umesema umebaini kuwapo kwa dosari 1,122 kwenye kampeni za vyama vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu.
Mwenyekiti wa Tacceo, Martina Kabisama alitaja baadhi ya dosari hizo kuwa ni wagombea kuzidisha muda na sera za vyama vyao, kutoleana lugha za kudhalilisha utu, kuzuiwa kufanya kampeni na vyombo vya dola, kuendesha kampeni za vitisho, vurugu na kauli za chuki. Nyingine ni matumizi ya rasilimali za umma, matumizi mabaya ya vyombo vya umma na vya habari, wananchi kuhongwa, kampeni kuendeshwa nyumba za ibada, uharibifu wa mabango, bendera na vifaa vya kampeni za vyama.
Alisema Tacceo imepokea kwa mshtuko maelekezo ya nyongeza ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu upigaji kura ya “kuruhusu watu ambao vitambulisho vyao havitakuwa na picha au vitakuwa na picha iliyofutika kuruhusiwa kupiga kura.”asia.”
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo Bisimba, aliitaka NEC kurekebisha maelekezo hayo ili kuepuka ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi kwa kuruhusu watu wasioruhusiwa kupigakura.
“Tunaitaka NEC itimize wajibu kwa kufuata sheria, taratibu, kanuni na maadili ya uchaguzi na kusimamia haki bila woga wala upendeleo,” alisema Dk Bisimba.

No comments :

Post a Comment