dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 22, 2015

Ukawa wajitabiria ushindi asilimia 61.

Mh. Edward Lowassa.
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimejipa uhakika wa kuibuka na ushindi wa jumla wa asilimia 61 katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili ijayo.
 
Ukawa unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD, umemsimamisha Edward Lowassa, wa Chadema kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Pia vyama hivyo kupitia Ukawa, vimeshirikiana kusimamisha wagombea wa ubunge, udiwani na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar.
 
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Ukawa na pia Chadema, Reginald Munisi, alisema baada ya kufanya tathmini yao ya ndani iliyowahusisha wapigakura 30,000 katika mikoa yote nchini, wamebaini kuwa watashinda kwa asilimia 61 na ndiyo maana hata wapinzani wao wamekuwa wakifanya mbinu mbalimbali za kukwamisha ushindi wao.
 
“Tunaamini kuwa ushindi wetu uko wazi na kwamba hivi sasa ndiyo maana kuna viashiria vinavyolenga kuwakatisha tamaa Watanzania kwa nia ya kuhujumu ushindi wetu,” alisema.Alidai kuwa baadhi ya viashiria ambavyo wanaendelea kuvidhibiti ni pamoja na kuwapo kwa njama za kukata umeme katika maeneo yote ambayo ni ngome yao hususan katika vituo vya kupigia kura na nyingine ni kuwapo kwa taarifa za mawasiliano mabovu ya simu ikiwamo mfumo wa data, sauti na  ujumbe mfupi wa maneno siku ya kupiga kura.
 
Hata hivyo, Ofisa Habari wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Adrian Severin, alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote.
 
MFUMO WA MATOKEO
Katika hatua nyingine, Munisi alisema wanaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuviruhusu vyama vya siasa kukagua mashine na mfumo mzima utakaotumika kujumulisha na kutangaza matokeo katika uchaguzi wa mwaka huu. 
 
Kwa mujibu wa Munisi, mfumo huo unajulikana kama Menejimenti ya Matokeo (Result Management System) ili kujiridhisha utendaji wake.
 
Munisi alisema hawana uhakika juu ya utendaji kazi wa mfumo huo na ndiyo maana wameiomba Nec iwashirikishe kuchunguza mfumo huo,  lakini hadi sasa hawajajibiwa  chochote.
 
Aidha, Munisi alisema wamepanga kukataa kutumia mfumo huo endapo hawatashirikishwa na kwamba msimamo wao zaidi juu ya hilo watautoa leo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment