dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

Utuluvi, amani ni muhimu siku ya kupiga kura

NA EDITOR

24th October 2015.
Katuni.
Kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika kesho nchini kote, kinamalizika leo kwa wagombea wa vyama mbalimbali katika nafasi za urais, ubunge na udiwani, kufunga kampeni zao za kujinadi.
 
Kipindi chote hicho Watanzania wameshasikiliza sera na ilani za vyama vyote na bila shaka wameshafanya maamuzi kwa kutumia vitambulisho vyao vya kupigia kura.
 
Tumekuwa tukikumbushwa mara kwa mara kuhusu kutunza vitambulisho vyetu vya kupigia kura hivyo katika siku hii iliyobaki ni muhimu kila mwananchi akahakikisha pale alipokihifadhi kiko salama na ni sahihi kwa matumizi.
 
Pamoja na misukosuko iliyojitokeza ya kupoteza wagombea katika siku za karibuni wakati tukielekea kumaliza kampeni hizi, bado tunaendelea tunamshukuru Mungu kwa utulivu ulioonyeshwa na wananchi katika kipindi chote hicho.
 
Ushabiki wa upinzani katika uchaguzi wa mwaka huu umekuwa mkubwa ukilinganisha na chaguzi zote za vyama vingi vya siasa ulivyowahi kufanyika miaka ya nyuma. Barabarani tumeona jinsi mashindano ya mabango, picha za wagombea na bendera za vyama zinavyoshindanishwa kupeperushwa.
 
Pamoja na ushabiki wote huo, lakini wananchi wameendelea kubishana kwa hoja na maisha yakiendelea kusonga mbele kwa sababu tunaelewa baada ya uchaguzi kuna maisha na watu wataendelea kuishi pamoja kama ndugu.  
 
Ni wajibu wetu sisi wananchi kuhakikisha kuwa kama tulivyoanza na kumaliza kampeni za uchaguzi, tuendelee kuwa watulivu hadi siku ambayo ni muhimu zaidi  tutakayosomewa matokeo ya washindi.
 
Ni matumaini yetu kuwa wananchi wataitumia siku hii muhimu kuhakikisha haki yao ya kupiga kura haipotei kwa kuzingatia mambo muhimu yaliyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
 
Katika siku hii moja iliyobaki, tuna imani kuwa kila Mtanzania atakuwa ametimiza wajibu wake wa kuhakiki kitambulisho chake cha kupigia kura ili mtu asipoteze haki yake ya kumchagua kiongozi anayeona anafaa kuongoza taifa hili.
 
Kwa mujibu wa NEC, wananchi wanapokwenda kupiga kura wanatakiwa kujiepusha na ushawishi wa aina yoyote ile, uwe wa kubebwa kwenye magari na kupelekwa kwenye vituo vya kupigia kura, kuvaa rangi za vyama vya siasa, nembo au bendera za vyama.
 
Kuvaa sare hizo kunaweza kuchangia mihemuko na kusababisha uvunjifu wa amani.
 
Kwa wale wenye vyombo vya usafiri vilivyobandikwa bendera au picha za wagombea ni vyema wakavibandua au kuviacha nyumbani ili kuwa katika hali salama.
 
Kadhalika mtu ambaye ameshapiga kura hatakiwi kuwatangazia wenzake kuwa amemchagua nani kwa sababu kura ni siri ya mtu na kufanya hivyo kunaweza kuleta mihemuko inayoweza kusababisha watu kutumia mwanya huo kuleta vurugu.
 
Kwa wale ndugu zetu wenye ulemavu wa viungo ukiwamo wa macho ni wajibu wakasaidiwa na ndugu zao wanaowaamini ili wasiweze kupoteza haki yao ya kumchagua wanayemtaka na siku hii ni muhimi ambayo hutokea mara moja katika kila kipindi cha miaka mitano.
 
Vyama vya siasa vina jukumu kubwa pia la kuwaelimisha wafuasi wake mambo muhimu wanayotakiwa kufanya na yasiyotakiwa katika siku hiyo ya kupiga kura.
 
Ni matarajio yetu kuwa wananchi wataitumia vema siku hii muhimu bila aina yoyote ya viashiria vya uvunjifu wa amani na vyombo vya usalama vitafanyakazi yake kwa kuzingatia misingi ya sheria bila upendeleo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment