dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 20, 2015

Wiki ya mwisho wananchi kuchambua chuya, mchele!

NA EDITOR

20th October 2015.
Katuni.
Kapeni za vyama vya siasa sasa zinaingia wiki ya mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili ijayo.
Bila shaka wagombea watatumia nafasi hii kunadi sera zao ili kuvutia wapigakura kabla ya uchaguzi huu unaotazamiwa kuwa wa kihistoria.
 
Ni mategemeo yetu kuwa wananchi nao watakuwa makini katika kusikiliza sera za wagombea wanaowania uongozi wa udiwani, ubunge na urais.
 
Tunachukua fursa hii kuwapongeza wagombea na wananchi kwa ujumla kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni zilizoanza Agosti 22, mwaka huu.
 
Kumekuwa na matukio machache ya vurugu, lakini zaidi wananchi wamekuwa watulivu katika kuwasikiliza wagombea wakinadi sera zao.
 
Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kuwa wa kihistoria kwani kwa mara ya kwanza kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya chama tawala CCM na vyama vya upinzani.
 
Kwa mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi urudishwe, nchi yetu inashuhudia uchaguzi wenye ushindani mkubwa zaidi. Hata hivyo, ushindani mkali umejitokeza kwa mara ya kwanza kwa upande wa Tanzania Bara tangu uchaguzi unaoshirikisha vyama vingi kufanyika mwaka 1995.
 
Tangu uchaguzi ulipofanyika kwa mara ya kwanza kwa kushirikisha vyama vingi kwa upande wa Zanzibar kumekuwa na ushindani mkali zaidi.
 
Bila shaka uchaguzi huu umekuwa na ushindani mkali zaidi kutokana na sababu nyingi.
 
Sababu mojawapo ni rika jipya la wapiga kura, ambao wengi wao ni vijana, wenye shauku kubwa ya kupiga kura kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha.
 
Wapigakura hawa wapya wanataka mabadiliko katika maisha yao, jambo ambalo limekuwa likipigiwa kampeni na wagombea wa vyama vyote.
 
Hata hivyo, wananchi walio wa kawaida nao wana shauku kubwa ya kushiriki uchaguzi huu wakiamini kuwa itakuwa fursa nzuri ya kuchagua viongozi watakaoendeleza gurudumu la maendeleo.
 
Ni dhahiri wananchi wanataka viongozi watakaokuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya taifa letu na hasa yale ya kupambana na umasikini, rushwa, ufisadi na ukosefu wa ajira. Tunashauri wananchi kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri kipindi hiki kilichobaki kuchagua viongozi makini wa  kukabiliana na matatizo ya taifa letu.
 
Ni vizuri sasa Watanzania kutumia vizuri kipindi hiki kilichosalia kuhakikisha wanawapima na kuwachambua wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.
 
Watanzania wanapaswa kuwa macho na watu wanaowania nafasi hizi za uongozi kwa ajili ya kujinufaisha.
Mathalani, kuna imani kuna watu wanaowania ubunge kwa fikra kuwa wakifika huko watanufaika kutokana na posho mbalimbali watakazozipata.
 
Ndiyo maana kuna wengine hufikia hatua ya kumwaga mamilioni ya fedha kwa kuwahonga wapigakura ili wafike bungeni kunufaika na fedha hizo.
 
Yafaa kuelewa kwamba fursa hii adhimu isipotumika vema kwa kuwachagua viongozi wanaofaa, basi tutaendelea kuwa nao hadi miaka mitano ijayo utakapofanyika uchaguzi mkuu mwingine. 
 
Ni kwa msingi huo basi ndipo tunawasihi Watanzania kuhakikisha kwamba wanatumia akili na utashi waliopewa na Mwenyezi Mungu kuwachagua viongozi wanaofaa ambao watalisukuma mbele gurudumu la maendeleo la Taifa letu.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment