Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 12, 2015

KOVA: TUNAMSHIKILIA MSHIRIKA WA LOWASSA


JESHI
la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini, imekiri kumshikilia mshirika wa aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Edward Lowassa, Bashiri Awale, kwa uchunguzi zaidi kwa kile kilichodaiwa uraia wake una utata.

Akizungumza Dar es Salaama jana katika mkutano wake na waandishi wa habari Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova, alisema; "Ni kweli tunamshikilia na kumchunguza Awale kutokana na tuhuma zinazomkabili."
Alisema inaonekana kuwa mtuhumiwa huyo ni raia wa Kenya na hata hati yake ya kusafiria namba C000529 inaonesha ni ya Kenya inayoonesha alizaliwa Julai 11,1969 jijini Nairobi.

"Ni kweli Jeshi la Polisi linamshikilia Bashiri Awale Mwanaharakati wa CHADEMA, ambapo mtu huyu tulimkamata Novemba 9, 2015 kutokana na tuhuma zinazoambatana na utata wa masuala mazima ya uraia wake na jinsi ambavyo amekuwa akijihusisha na masuala ya kisiasa nchini Tanzania," alisema Kamanda Kova.Alisema mbali na pasi hiyo ya kusafiria kuonesha ni raia na mzaliwa wa Kenya katika Jiji la Nairobi, lakini baada ya kukamatwa na kupekuliwa nyumbani kwake eneo la Mikocheni alikutwa na cheti cha kuzaliwa namba D063711 kwa jina la Bashiri Abdi Ally kilichoonesha amezaliwa Julai 11,1969 katika Hospitali ya Serikali mkoani Dodoma, nchii Tanzania.

Alisema kumbukumbu hizo zinazokinzana zimeleta utata, hivyo wanaendelea kumhoji kwani kwa na uraia wa nchi mbili ni kosa chini ya sheria za uhamiaji.
Alisema zipo tuhuma zinazonesha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akijihusisha kikamilifu na siasa za Tanzania hususan katika kipindi cha uchaguzi uliomalizika, jambo ambalo ni kinyume na katiba mwaka ya Tanzania ya 1977.

Aliongeza kuwa Katiba ya Tanzania haimpi nafasi mgeni yeyote kuchagua,kushiriki katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani na inatoa haki kwa raia husika kushiriki kikamilifu uchaguzi huo.
Majira

No comments :

Post a Comment