Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 12, 2015

Magufuli kuibukia U/Taifa Jumamosi

  Baada ya kufanya ziara za kushtukiza Wizara ya Fedha na Hospitali ya Taifa Muhimbili, mkuu huyo wa nchi atatinga kwenye uwanja huo kuishuhudia Stars dhidi ya Algeria

Rais mpya wa Tanzania, John Magufuli.
Rais mpya wa Tanzania, John Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya Taifa Stars dhidi ya Algeria keshokutwa, imeelezwa.
 
Mechi hiyo ya kwanza ya kusaka timu itakayotinga hatua ya makundi matano kuwania kupata timu tano za Afrika zitakazofuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, aliwaambia waandishi wa habari jijini jana kuwa Rais amepanga kuwa miongoni mwa watu watakaohudhuria kwenye Uwanja wa Taifa siku hiyo kuishuhudia mechi hiyo ya kwanza ya kimataifa kuchezwa kwenye uwanja huo tangu ashike madaraka hayo makubwa.
 
"Kama hakutakuwa na mabadiliko, Rais Magufuli atakuwapo uwanjani kuwapa sapoti wachezaji wetu wa timu ya taifa ili wafanye vizuri katika mchezo wao dhidi ya Algeria," alisema Sadiki.
 
Alisema anatumaini nyota wa Stars hawatamuangusha Rais Magufuli siku hiyo kutokana na maandalizi waliyofanya wakiwa kambini Afrika Kusini."Mimi kama mlezi wa Kamati ya Saidia Taifa Stars na timu kwa ujumla ninaamini wachezaji hawatamuangusha Rais, watapambana na kupata ushindi dhidi ya Algeria," alisema zaidi Sadiki huku akitroa rai kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao.
 
Sadiki pia aliwapongeza washambulia wa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa kuisaidia klabu yao ya TP Mazembe kutwaa taji la tano la Klabu Bingwa Afrika Jumapili iliyopita.
 
"Tunawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani na hatutawaangusha, suala la ushindi na ubingwa wa TP Mazembe kwa sasa tunaweka pembeni na akili zote tunazielekeza kwenye mchezo dhidi ya Algeria," alisema Samatta aliyekuwa amefuatana na Ulimwengu wakati wa mkutano wa Sadiki na waandishi wa habari.
 
Jumatatu Stars itasafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Novemba 17 nchini humo.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya  Dar es Salaam limesema litaimarisha ulinzi na usalama wakati wa mechi ya keshokutwa.
 
Suleiman Kova, Kamada wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, aliwaambia waandishi wa habari jijini jana kuwa wamejipanga kuhakikisha mashabiki wanaangalia mechi hiyo kwa amani na utulivu.
 
"Kutakuwa na kamera maalum zitakazokuwa zinaangalia uwanjani, chochote kitakachofanyika kitaonekana na wahausika (wasiotii sheria na taratibu) watachukuliwa hatua kali za kisheria," alisema Kova.
 
Alisema tayari jeshi hilo limelishauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanza kutoa adhabu dhidi ya mashabiki wanaobainika kufanya vitendo vya kihuni viwanjani na vyenye kuhatarisha amani kama mashirikisho na vyama vingine vya soka vya nchi nyingine zinavyofanya.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment