dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 19, 2015

Majaliwa athibitishwa na Bunge, rasmi ni Waziri Mkuu Mteule

Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa akipongezwa na wabunge kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
By Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Dar es Salaam. Wabunge wamemthibitisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kura 258 kati ya 351 zilizopigwa. Uthibitisho huu ni wa asilimia 73.3. Wabunge wamepiga kura ya kumthibitisha baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais John Magufuli na kuliwasilisha jina hilo bungeni leo asubuhi.
Kufuatia kuthibitishwa kwake, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Waziri Mkuu huyo mteule ataapishwa saa nne asubuhi kesho, Ikulu ndogo iliyopo Chamwino, mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, wabunge 91 sawa na asilimia 25.9  walipinga uteuzi huo na kura mbili ziliharibika.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah amesema jumla ya wabunge wote 394 waliosajiliwa, ni 369 tu walioshiriki uteuzi huo, idadi ambayo inakubalika kisheria kufanya uamuzi.
Akitangaza kuthibitishwa kwa Waziri Mkuu mteule, Spika wa Bunge Ndugai alimpongeza kwa kuaminiwa na Rais pamoja na Bunge. Amemuahidi yeye na mawaziri wake ushirikiano wa dhati katika kuwatumikia watanzania.
Historia ya Majaliwa inaonyesha alizaliwa Disemba 22, 1960 na kupata elimu katika Shule ya Msingi Mnacho kati ya mwaka 1970 na1976 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Kigonsera kati ya mwaka 1977 na 1980.
Mwaka 1991-1993, alijiunga na Chuo cha Ualimu Mtwara. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1994 na kuhitimu mwaka 1998 kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden kwa masomo ya juu.
Amehudumu katika nafasi mbalimbali tangu mwaka 1984 alipojiunga na utumishi wa umma kama mwalimu mkoani Lindi, Katibu wa Chama cha Walimu wa Wilaya, Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa na baadaye  Mkuu wa Wilaya.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kabla ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumteua mwaka 2012 kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.

No comments :

Post a Comment