Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 12, 2015

Vita vya uspika kama urais CCM

Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Vitu ya kuwania uspika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) haina tofauti na vita vya kuwania urais kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 
 
Mpambano wa kuwania uteuzi wa kugombea urais kupitia CCM ulijumuisha makada 42 ambao walichukua fomu, lakini waliozirejesha na kutimiza masharti ni 38.
 
Mchuano wa kuwania nafasi ya uspika kwa ajili ya kuliongoza Bunge la 11 ambao milango yake ilifunguliwa jana ndani ya CCM kwa makada wake kuanza kuchukua fomu unaonekana kufanana na wa mbio za urais kutokana na wengi kuuchangamkia.
 
Makada tisa walijitokeza jana ikiwa ni siku ya kwanza ya uchukuaji wa fomu, hali inayoashiria kuwa hadi kufungwa kwa mchakato huo Jumapili, idadi kubwa itajitokeza.
 
Uchukuaji wa fomu hizo ulifanyika katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM Taifa (Oganaizesheni), Dk. Mohamed Seif Khatibu, aliwakabidhi wagombea hao wote fomu kwa nyakari tofauti kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 10:00 jioni.
 
MAKADA WALIOJITOSA
Aliyefungua pazia la uchukuaji fomu saa 6:00 baada ya chama hicho kufungua milango ni aliyekuwa Spika wa Bunge la tisa na Waziri wa Uchukuzi katika serikali ya wamu ya Nne iliyomaliza muda wake, Samuel Sitta. Sitta pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.Wengine ni Balozi wa zamani wa Tanzania Italia na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Prof. Costa Mahalu; aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi.
 
Makada wengine ni Mbunge wa zamani wa Afrika Mashariki, George Nangale na waliokuwa katika kinyang’anyiro cha kuomba uteuzi wa kugombea urais 
Leonce Mulenda na Muzamil Kalokola. Wamo pia Banda Sonoko na Simoni Rubugu. 
 
Naibu Spika mstaafu, Job Ndugai, juzi aliithibitishia Nipashe kuwa ataomba ridhaa ya chama chake kumteua kugombea nafasi hiyo na kueleza kuwa uzoefu, elimu na uwezo wa kazi vinamuwezesha kumudu nafasi hiyo.
 
Pamoja na hao waliojitokeza jana na kuchukua fomu, makada wanaotajwa kuwa wana nia ya kuwania nafasi hiyo ya kuliongoza Bunge la 11 ni aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda na Mwenyekiti wa Bunge la 10, Mussa Azan Zungu.
 
Alipoulizwa na Nipashe, Zungu alisema anasubiri utaratibu wa Chama, na alipoelezwa kuwa chama kimeshatoa ratiba alisema anaelekea kwenye ofisi za Chama kujua utaratibu zaidi.
 
CCM YATOA RATIBA
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano na Umma cha Idara ya Itikadi na Uenezi cha CCM, utaratibu wa uchukuaji fomu kwa wanachama na wabunge wateule katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa utaratibu huo, wanachama wa Chama hicho walielekezwa kuchukua fomu kuanzia jana saa 6:00 mchana na wataendelea kuzichukua leo kisha kuzirejesha leo kabla ya saa 10:00 jioni.
 
Kuhusu wabunge wateule, CCM imeelekeza kwamba wataanza kuchukua fomu leo na wanatakiwa kuzirejesha Jumamosi kabla ya saa 10:00 jioni.
 
Hata hivyo, taarifa hiyo haikufafanua vikao vya mchujo wa kubakisha jina moja la mgombea wa nafasi ya Spika na Naibu, vitakutana lini.
 
Kwa mujibu wa utaratibu uliyotolewa na ofisi ya Bunge, majina ya wagombea kwa kila chama yanatakiwa kuwasilishwa siku mbili kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge Novemba 17, mwaka huu.
 
Kwa wanachama wa kawaida wanaogombea nafasi hizo ni lazima majina yao yapelekwe Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwa ajili kuangalia kama wana sifa za wabunge au la.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Nec, Emmanuel Kawishe, alipoulizwa kama kuna fomu zimeshapelekwa, alisema hawajapokea fomu yoyote.
 
Kwa mujibu wa utaratibu uliotangazwa mwanzoni mwa mwezi huu na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, Ofisi ya Bunge itapokea majina ya wagombea kutoka kwenye vyama siku mbili kabla ya Bunge kuanza. Bunge litaanza Novemba 17, hivyo majina yanatakiwa kufika Novemba 15.
 
Kadhalika, Ofisi hiyo imevitaka vyama kuwasilisha majina hayo ikiwa ni pamoja na kupeleka Nec majina ya wagombea ambao ni wanachama ili yakaguliwe kama wana sifa za kuwa wabunge.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment