dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 19, 2015

Wasomi waamini Ndugai atamudu changamoto

Spika wa Bunge, Job Ndugai    

By Joyce Mmasi, Mwananchi
Spika wa Bunge, Job Ndugai anatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumudu changamoto zinazolikabili Bunge la Kumi na Moja kutokana na uzoefu alioupata alipokuwa Naibu Spika miaka mitano iliyopita. Wakizungumza jana, wachambuzi wa masuala ya siasa nchini wamemwelezea Ndugai kuwa mgombea aliyestahili ushindi wa nafasi hiyo.
“Ni wazi kuwa Bunge lijalo ni gumu, lakini Ndugai si mgeni. Litakuwa Bunge la kibabe lakini Ndugai naye ni mbabe… anazo sifa za ziada na uzoefu wa kuendesha Bunge la wabunge matata, naamini atamudu vyema changamoto atakazokutana nazo,” anasema Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM), Kitila Mkumbo.
Hata hivyo, Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dk Alexander Makulilo alisema ili amudu changamoto zinazolikabili Bunge la Kumi na Moja, Ndugai anatakiwa kusimama imara na kuhakikisha anaendesha Bunge bila upendeleo wala kujali itikadi za vyama vya siasa. 
Dk Makulilo alisema Bunge lijalo linakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wabunge wapya na vijana na kuwa ili kuendana na kasi ya Bunge hilo, Ndugai anapaswa kuliendesha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na kuweka kando masilahi ya chama chake.
“Ndugai si mgeni wa haya mambo, amekuwa naibu spika kwa muda mrefu, anao uzoefu mkubwa tu, hatazamiwi kuwa ni mpya katika nafasi hiyo… kazi yake itakuwa nyepesi endapo atatimiza wajibu wake, aendeshe Bunge bila upendeleo, asichukue upande. Bunge lisiwe na itikadi za vyama,” alisema Dk Makulilo. Alisema mbali na spika, wabunge wanapaswa kutambua kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi hivyo wajibu wao ni kuwatetea na kuwasemea na kuachana na itikadi za kisiasa. Alisema endapo spika au wabunge watatoka kwenye mstari wa kusimamia masilahi ya Taifa na kukumbatia ya vyama vyao, wataifanya kazi yao ya uwakilishi wa wananchi kuwa ngumu na watashindwa kuiwajibisha Serikali pale inapobidi.
“Wabunge wakipatiwa mafunzo na wote kwa ujumla wao wakizijua na kuziheshimu kazi zao, kamwe spika hawezi kupata na shida kubwa katika kuliongoza Bunge,” alisema, Alisema wabunge na spika wanayo nafasi ya kurejesha heshima iliyopotea ndani ya chombo hicho muhimu kwa kila mmoja kuzingatia nafasi aliyopewa ni ya uwakilishi wa wananchi wake hivyo anapaswa kuitenda haki.
Mkurugenzi wa Fordia, Buberwa Kaiza alisema Watanzania wasitegemee kitu kipya katika uongozi wa Ndugai bungeni kwa maelezo kuwa atafanya kazi kwa masilahi ya chama tawala ambacho ndicho kilichompa nafasi hiyo.
Alisema Ndugai hajaanza uongozi wa bungeni mwaka huu akisema alikuwa mwenyekiti wa kamati kwenye Bunge la Tisa, naibu spika Bunge 10 na sasa spika hivyo ni mzoefu na anayejua wajibu uliopo mbele yake.  

No comments :

Post a Comment