Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 19, 2015

Bomoa bomoa Dar kuliza zaidi ya watu 2,000

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
Zaidi ya nyumba 400 zenye wakazi wasiopungua 2,000 ambazo zimejengwa mabondeni jijini Dar es Salaam, zinatarajiwa kubomolewa. Kazi ya ubomoaji wa nyumba hizo ilianza rasmi jana katika bonde la Mkwajuni kata ya Hananasif wilayani Konondoni ambako katika bonde hilo la Mto Msimbazi, jumla ya nyumba 100 zitavunjwa na nyingine zaidi ya 300 eneo la Magomeni.
 
Kazi ya kubomoa nyumba hizo inafuatia ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aliyoifanya juzi katika maeneo ya mabondeni.
 
Akiwa katika ziara hiyo, Mhagama alishangazwa agizo la Rais mstaafu Jakaya Kikwete, la nyumba hizo kubomolewa kupuuzwa. Kazi ya ubomoaji wa nyumba hizo ilianza jana saa 4:30 asubuhi na kusimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira nchini (Nemc) huku ikiibua vilio kwa wakazi wa eneo hilo baada ya kupewa dakika 15 za kuondoa mali zao nje ya nyumba ili zivunjwe.Mwanasheria wa Nemc, Manchare Suguta, alisema shughuli hiyo ni ya siku 30 ambayo itakayohusisha pia bonde la Mto Msimbazi kata ya Hananasif ambako zitavunjwa nyumba zaidi ya 100 na Magomeni zaidi ya 300.
 
“Tunachotaka hawa watu warudi kwenye viwanja vyao walivyopewa na serikali, haya siyo maeneo salama kwa ajili ya afya zao na mazingira kwa ujumla. Tunatoa wito kwa Watanzania wanaojifahamu kuwa wanaishi katika maeneo ya kingo za mto ama bahari, waondoke mara moja na watafute sehemu ambayo inakubaliwa. 
 
Kazi hii itafanyika nchi nzima,” alisema. Alisema kazi hiyo itaendelea eneo la Jangwani na wale wote wanaozungukwa na mto Msimbazi na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 yaliyopo jijini Dar es Salaam.
 
VILIO VYATANDA UBOMOAJI
Mayowe, vilio na simanzi vilitawala miongoni mwa wakazi ambao nyumba zao zilianza kuwa maeneo ambako kazi ya ubomoaji ilianza huku wakiitupia lawama serikali.
 
“Kuliko ubomoe nyumba yetu, ni bora utuue sisi. Hatuna pa kwenda, mmekuja kuvunja bila ya taarifa, jambo hili halikubaliki,” alisema Maimuna Samson, wakati tingatinga likiendelea kuvunja  nyumba yao.
 
Naye Khadija Athumani, alisema juzi viongozi wa Manispaa ya Kinondoni walikwenda kuangalia eneo hilo, lakini hawakuwaeleza kuhusiana na operesheni hiyo.
 
Alisema serikali inadai kuwa iliwapa viwanja Mabwepande, lakini walikuwa hawajawapatiwa, jambo linalowafanya washindwe kuhama eneo hilo.
 
 Kwa upande wake, Mjumbe wa Shina namba 19 wa eneo hilo, Peter Kanji, alihoji sababu ya serikali kuwa kimya kipindi chote kwani eneo hilo wameishi kwa miaka zaidi ya 30. Kwa upande wake, Ofisa Mipango Miji wa Ardhi, Dk. Charles Mkalawa, alisema Sheria ya Mpango kabambe ya mwaka 1979, inasema eneo hilo ni hatarishi na Nemc iliwakataza watu kuishi karibu na mito.
 
Alisema watu wanatakiwa kuishi umbali wa mita 60 kutoka katika vyanzo hivyo.
 
Mei 14 mwaka huu, Rais mstaafu Kikwete, alifanya ziara  eneo la Jangwani na bonde la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kuagiza wakazi wa maeneo hayo wahame, lakini agizo hilo halikutekelezwa. Hatua hiyo ilimshutua Waziri Mhagama aliyefanya ziara juzi katika eneo la Boko Basihaya na Buguruni ambako wakazi wake wamekumbwa na mafuriko.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment