AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 10, 2015

MHE.BALOZI WILSON M. MASILINGI ATEMBELEA KITENGO CHA VISA KATIKA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON D.C, SIKU YA KUMBUKUMBU YA UHURU, TAREHE 9 DISEMBA, 2015

 
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kulia) akipolewa na Bw. Abass Missana, Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji.
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na wafanyakazi wa kitengo hicho. Kulia ni Bi. Swahiba H. Mndeme, Mkuu wa Utawala na Fedha, Ubalozini.
Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na Bi. Mariam Mkama, Mtumishi wa Ubalozi, kitengo cha Visa
Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na mmoja wa wateja wa Visa aliyefika Ubalozini kupata huduma hiyo
Mhe. Balozi Masilingi akizungumza na Bw. Arnold NzuaMtemi Nzali wa Las Vegas, Nevada aliyefika Ubalozini kupata huduma ya Pasipoti.

Katika kutekeleza agizo la Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington D.C umendelea kufanya kazi na kutoa huduma za Visa na Pasipoti kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu hiyo.

Pamoja na kazi zingine za Ubalozi kuendelea kama kawaida, Mhe. Balozi Wilson M.Masilingi alitembelea kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na kufanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa Kitengo hicho Bw. Abbas A. Missana, Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi, (Minister Plenipotentiary).Katika Mazungumzo hayo, Bw. Missana alimweleza Mhe. Balozi kuwa kumekuwa na ongezeko la wageni wanaokuja Ubalozini kuchukua Visa, mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 kumalizika salama. Hapo awali, kabla ya uchaguzi idadi ya wageni waliokuwa wanafika Ubalozini kuomba Visa ilipungua kwa kiasi kikubwa.

Mhe. Balozi aliwapongeza Wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuitikia wito wa “Uhuru na Kazi” kwa hamasa kubwa, jambo linalodhihirisha uzalendo na kuheshimu miongozo sahihi toka kwa Mkuu wa Nchi na wasaidizi wake. Aidha, aliwataka Watumishi wa Ubalozi kuendelea kuboresha huduma kwa wateja ili kulinda heshima ya nchi yetu.

/Vijimambo.

No comments :

Post a Comment