Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 23, 2015

Muhongo aonja adha ya kukatika umeme

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
Wakati Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akiliagiza Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kuacha ‘mchezo’ wa kukata umeme kila wakati, jana waziri huyo alionja adha hiyo alipofanya ziara ya kukagua mitambo ya uzalishaji umeme mkoani Mwanza.
 
Umeme jijini Mwanza ulikatika maeneo mbalimbali huku waziri huyo hivi karibuni akiwaagiza watendaji wake kuacha tabia ya kukata umeme pasipo sababu. Akiwa katika ukaguzi wa mitambo hiyo saa 3:30 hadi saa 5 asubuhi, Prof. Muhongo alitoa agizo kwa shirika hilo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja linamaliza mgogoro kati yao na mkandarasi aliyetengeneza mitambo ya uzalishaji wa umeme mkoani Mwanza ulioharibika ndani ya miaka miwili.
 
Akitoa agizo hilo jana katika mkongo mkubwa wa umeme uliopo Nyakato unaohudumia mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mara, Mwanza na Geita, alisema wananchi wanatakiwa kupata umeme wenye megawatts 80, endapo mitambo hiyo mitatu ikitengenezwa na kufanya kazi, tatizo la umeme litaisha.
 
“Kufikia mwezi ujao, lazima mhakikishe mnamaliza mgogoro na Ubalozi wa Denmark na Norway kutokana na mikataba mliyowekeana kuonyesha ni mibovu na kusababisha  matatizo ya kutupiana mizigo ya uharibikaji wa mitambo hiyo mitatu. Waliokuwa makandarasi wakati wa utengenezaji ni lazima wachukuliwe hatua,” alisema Prof. Muhongo. Aidha, aliwataka wawe makini na akandarasi na siyo kuweka watu wababaishaji wa kuleta vifaa vibovu.
 
Aidha, alitaka apewe maelezo ya kina juu ya deni la Dola 300 za Marekani wanazodaiwa ambalo linaweza likasababisha wananchi wakakosa umeme.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment