Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 22, 2015

Tiketi Ubungo kizungumkuti

xmassNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM, MTANZANIA.
ABIRIA waliotaka kusafiri kwenda wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, nusura wachapane ngumi wakigombea foleni ya kukata tiketi katika Kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo (UBT).
MTANZANIA lilishuhudia abiria hao wakiwa kwenye foleni wakisubiri kukata tiketi katika mabasi ya Kampuni ya Meridian yanayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Rombo mkoani Kilimanjaro.
Katika tukio hilo, baadhi ya abiria walivuruga utaratibu wa foleni kwa kuwavuka wenzao na kujisogeza mbele ili wakate tiketi, hali iliyosababisha kutoelewana miongoni mwao, huku wengine wakitoleana matusi wengine wakitaka kurusha ngumi.
“Msituchanganye bwana, kama vipi hapa ngumi zitapigwa, sisi tumepanga foleni wao wanataka kujifanya wana haraka sana wanavuruga foleni kwa kujipeleka mbele,” alisikika dada mmoja akilalamika huku wakatishaji wa tiketi za kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa wakichukizwa na hali hiyo wakida inawazuia kufanya kazi zao kwa uhuru.
Mfanyakazi wa Kampuni ya mabasi ya Osaka yanayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Musoma, aliwalaumu abiria wanaokwenda mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuwa wamekuwa kero kutokana na kung’ang’ania katika kituo hicho licha ya kuambiwa tiketi za kwenda katika mikoa hiyo zimekwisha.
“Yani hawa abiria wa Rombo wamekuwa kero sana, wanatufanya sisi tushindwe kufanya kazi kwani hawaamini kuwa tiketi zimekwisha wao wanang’ang’ania maofisini tu,” alisisikika akilalamika.
Abiria mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Elisha Ngowi, alisema kuwa tangu juzi alifika kituoni hapo kwa ajili ya kukata tiketi kwenda Rombo, lakini mawakala wa basi la Meridian walimtaka aondoke arudi siku iliyofuata.
Upatikanaji wa tiketi katika kituo hicho umekuwa kama donda ndugu kwani kila mwaka kuelekea Sikukuu ya Krismasi watu wengi hutaabika kutokana na usafiri wa kwenda katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments :

Post a Comment