
Amlitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nangurugai, kata ya Mbwemkuru, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, ambako alikwenda kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja za Diwani wa Nangurugai, Selemani Likuche, aliyetoa ombi la kutengenezwa kwa daraja hilo kutokana na kukata mawasiliano baina ya kijiji hicho na wilaya ya Liwale.
Pia aliomba wapatiwe dawa na watumishi kwenye zahanati yao.
Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema kazi ya ujenzi wa daraja hilo itakamilishwa haraka. Pia aliitaka Halmashauri ya Ruangwa isimamie uboreshaji wa barabara ya kutoka Nangurugai hadi Chikwale yenye urefu wa kilomita 35 kwa sababu ni muhimu kwa kusafirisha mazao katika eneo hilo.
“Hili eneo ni maarufu kwa zao la ufuta, kwa maana hiyo linaongeza pia mapato ya halmashauri, simamieni hii barabara ili wananchi wasisumbuke kuuza mazao yao,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa, Nicholas Kombe, alisema milingoti ya daraja hilo ilikwishajengwa na kinachosubiri ni kupokea vyuma vya kutandaza juu ya daraja.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa kwenye zahanati yao, Majaliwa alisema ameshazungumza na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo ambaye amemhakikishia kuwa ameanza maboresho ya upatikanaji dawa katika zahanati zote.
Kuhusu tatizo la watumishi wa sekta ya afya, aliahidi kuwa watapatikana katika muda mfupi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment