.png)
Serikali ya Awamu ya nne ilikuwa ikikusanya Sh. bilioni 900 kila mwezi.
Ahadi hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (pichani), alipokuwa akiwahutubia wakazi wa mji wa Lindi jana akiwa katika ziara yake ya siku ya kwanza jimboni mwake.
“Wakati tunaanza kuziba mianya ya wezi, kuna baadhi walianza kutaka kutugombanisha na wafanyabiashara. Serikali ya awamu ya tano haina mpango huo,” alisema.
Waziri Mkuu alisema serikali yake itahakikisha inafikia makusanyo hayo kila mwezi ili kutimiza malengo iliyojiwekea.
Awali akisoma risala ya Mkoa wa Lindi, Mkuu wa mkoa huo, Jordan Rugimbana, alisema moja ya kero kubwa inawatesa wakazi wengi wa mkoani humu ni ukosefu wa maji safi na salama.
“Upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 45.6 wakati mijini ni asilimia 57.8 na asilimia 81.2 ya wakazi wote 864,653 wanaishi vijijini,” alisema.
Rugimbana alisema hali hiyo ni tofauti na takwimu za kitaifa zinazosema wakazi wa mijini wanapata maji kwa asilimia 86.
Akijibu risala hiyo, Waziri Mkuu alisema uhaba wa maji umechangiwa na kusuasua kwa mradi mkubwa wa Ng’apa kwa kukosa fedha ambapo serikali ya sasa itahakikisha inaukamilisha.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment