Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 6, 2016

Balozi wa Italia ampa 'tano' Magufuli

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luig Scotto
Balozi wa Italia nchini Tanzania,  Luig Scotto, amepongeza juhudi za utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli katika kuleta mabadiliko ya kweli ambayo Watanzania walikuwa wakiyataka.
 
Scotto, ambaye ni kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, alisema Dk. Magufuli ameonyesha njia ya kweli katika utendaji wake wa kazi.
 
Balozi huyo alisema katika ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana,  aliahidi mambo mengi ambayo ameanza kuyafanyia kazi.
 
Aliyasema hayo hivi karibuni akiwa mkoani Iringa  baada ya kukabidhi hundi ya sh. milioni 20 kwa Shule ya Sekondari ya Nyerere iliyoko  Migoli, Isimani  mkoani Iringa.
 
Shule hiyo ambayo ni ya kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, ilijengwa na Kanisa Katoliki kwa usimamizi wa Padre Salvatory Ricceri aliyekuwa Paroko wa Migoli wakati huo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment