Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 6, 2016

Dk. Shein awapa neno watumishi wa afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka watumishi wa sekta ya afya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na taaluma.
 
Akizungumza katika hafla ya kuweka mawe ya msingi ya majengo ya huduma za wazazi na watoto katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja jana, Dk. Shein alisema katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake, maendeleo ya sekta ya afya yameongezeka na kuifanya Zanzibar kupiga hatua kubwa katika kada hiyo. 
 
Alisema azma ya kuzipandisha hadhi hospitali za Mnazi Mmoja na ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba pamoja na hospitali za Koteji Unguja na Pemba kuwa za wilaya, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa na wananchi wanapaswa kujivunia mafanikio hayo.
 
“Tumeongeza huduma mbalimbali katika hospitali ya Mnazi Mmoja kama vile kuanzisha idara za saratani, magonjwa ya njia ya chakula, kusafisha damu, upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo na nyinginezo. Majengo  yaliyowekwa mawe ya msingi ni mwendelezo wa hatua hizo,” alisema.Dk. Shein alisisitiza kuwa azma ya serikali ya kuiwezesha hospitali ya Mnazi Mmoja kutoa huduma za upasuaji wa moyo iko pale pale na kwamba utekelezaji wake utaanza hivi karibuni. 
 
Alibainisha kuwa Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika kuweka mtandao wa miundombinu ya afya na utoaji wa huduma pamoja na kuwa ziko changamoto kadhaa katika kufikia ubora na malengo yaliyowekwa.
 
“Ni kweli tunakabiliwa na changamoto nyingi katika utoaji wa huduma za afya lakini changamoto hizo zisiwafanye wenzetu wengine kuyabeza mafanikio haya tuliyoyapata,” alisema.
 
Alibainisha kuwa hatua zilizochukuliwa kuzipandisha hadhi hospitali hizo ni pamoja na kuzipatia vifaa bora na vya kisasa na wataalamu wanaotakiwalicha ya kuwepo upungufu wa majengo ambao serikali inakabiliana nao hatua kwa hatua.
 
Majengo aliyoweka mawe ya msingi, ikiwa sehemu ya maadhimisho miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ni la wazazi na watoto wachanga ambalo litakuwa na wodi ya kinamama, vyumba vya upasuaji, vyumba vya kujifungulia, sehemu ya huduma za dharura na huduma zingine muhimu za kitabibu.
 
Jengo lingine ni la watoto wadogo litakalokuwa na wodi ya vitanda 100 kati yake 32 ni kwa watoto wenye magonjwa ya kuambukiza, 54 ya watoto wasiokuwa na magonjwa ya kuambukiza na 10 kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma za kusafisha figo.
 
CHANZO: NIPASHE

1 comment :

  1. Kwa kujisifu tu wako mstari wa mbele lakini nenda ukayaangalie mazingira ya hizo hospitali, ukiingia kama mgonjwa basi maradhi yatazidi. Hakuna dawa, hamna huduma nzuri ,yaani kila kitu majanga tu

    ReplyDelete