By Florence Majani, Mwananchi
Dar es Salaam: Mwanasheria wa kujitegemea nchini, Fatma Karume amemshauri Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein kuachia madaraka.
“Dk Shein lazima aondoke kwa sababu kuendelea kubaki madarakani ni kuwanyang’anya Wazanzibari haki yao ya msingi,” alisema Fatma ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Fatma alisema kuwa mzozo wa Zanzibar umesababishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kutangaza kufutwa matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu visiwani humo wakati hana mamlaka kisheria kufanya hivyo.
Fatma alisema Jecha hana mamlaka kikatiba na kisheria kufuta matokeo hayo kwa kuwa maamuzi kama hayo yanatakiwa kufanywa na ZEC yenye mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe watano; watatu kutoka CCM na wengine wawili kutoka CUF.
“Akidi ya vikao vya ZEC ni mwenyekiti na wajumbe wanne. Kama kikao kilifanyika, akidi ilitimia na jambo hilo likakubaliwa na tume hiyo, basi waonyeshe ni wapi walipokubali wajumbe wengine. Hata makamu mwenyekiti hajashiriki kwenye maamuzi hayo kwa sababu kisheria uchaguzi hauwezi kufutwa bila kupata akidi hiyo,” alifafanua Fatma.
Mwanasheria huyo alisema kuwa amekuwa akiwasikia baadhi ya wana CCM Zanzibar wakisema kuwa Jecha ndiyo tume na tume ndiyo Jecha, hivyo ana haki ya kufuta uchaguzi. Lakini Fatma alisema Jecha hana mamlaka kusema jambo ambalo halijakubaliwa na tume.
Alipoulizwa ikiwa hatua ya aliyekuwa mgombea urais kupitia CUF, Seif Sharrif Hamad ya kutangaza matokeo aliyodai yalimpa ushindi si kosa, Fatma alisema, “Sikumuona Maalim Seif alipokuwa anatangaza matokeo hayo hivyo sijui kama alijitangaza kuwa mshindi au alitangaza matokeo kama yalivyobandikwa kwenye vituo.
“Katika nchi zilizokomaa kidemokrasia mgombea anaweza kuona mwelekeo wa matokeo na akampigia mwenzake kumpongeza. Nadhani Maalim Seif alisoma jumla ya matokeo ya uchaguzi kama yalivyobandikwa kwenye vituo, hivyo hilo si kosa ati,” alisema na kuongeza: “Ninasikitishwa na tabia hii. Sikutegemea kama CCM watatumia nguvu kutaka kubaki madarakani kwa njia hii. Sikutegemea kama watavuruga katiba…ndiyo maana nina huzuni.”
Jambo jingine alilosema litazua mgogoro Zanzibar ni mamlaka yenye haki ya kuidhinisha fedha za uchaguzi wa marudio ikiwa watalazimisha ufanyike.
“Kisheria fedha hizo ni lazima zikubaliwe na Baraza la Wawakilishi. Baraza lipo wapi? Ili mtu awe waziri lazima awe mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. Rais alivunja Baraza Agosti na kwa hiyo hadi ilipofika siku ya kuapishwa rais mpya, Zanzibar hakuna Baraza wala Waziri. Ina maana fedha za wananchi zinatumiwa bila idhini ya Baraza, ” alisema.
Alisema kinachofanyika Zanzibar ni ‘ukoloni’ wa watu weusi dhidi ya watu weusi ambao unawakosesha Wazanzibari haki yao msingi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.
“Hali si shwari Zanzibar. Watu wamekata tamaa kwa sababu unapokuwa na Serikali ambayo inanyang’anya haki ya wananchi ya kupiga kura, kuandamana, watu wanakosa imani na Serikali hiyo,” alisema.
Kurudia uchaguzi
Kuhusu kurudiwa uchaguzi nchi nzima, Fatma alisema ulipofanyika uchaguzi mwaka 2000 ambao Amani Karume aligombea kwa mara ya kwanza, zilitokea dosari katika majimbo 10 ya Unguja. CUF walipotaka uchaguzi urudiwe nchi nzima, CCM chini ya Benjamin Mkapa waligoma wakasema ni katika majimbo yenye dosari tu.
“Nini kimetokea mwaka huu? Kama dosari zilijitokeza Pemba kama wanavyodai kwa nini urudiwe Unguja? Kwa nini hawataki kutumia uamuzi wa mwaka 2000 wa kurudia maeneo yenye dosari tu?” alihoji.
“Mkapa alisema wazi kwenye kipindi cha Hard Talk cha BBC akihojiwa na mtangazaji Tim Sebastian uchaguzi hauwezi kufutwa ila utarudiwa tu katika baadhi ya majimbo. Kwa nini leo mambo yamebadilika na CCM inataka uchaguzi mpya?” alihoji.
Fatma ambaye alikataa kueleza msimamo wake kisiasa, alisema iwapo uchaguzi huru na wa haki utafanyika leo Zanzibar, CCM haiwezi kushinda kwa sababu Wazanzibari wanajionea yale ambayo wanafanyiwa na chama hicho.
“CCM imeshindwa Zanzibar kwa sababu ilishindwa kuwashawishi watu wake na badala inawakemea, ikawanyima haki zao. Kisaikolojia wapiga kura wanataka haki zao na wasibaguliwe lakini ukiwapelekea jeshi na vifaru, unazidi kuwapoteza,” alisema.
Sherehe za Mapinduzi
Wakati zikiwa zimesalia siku nne kufikia kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, Fatma alisema kwa hali ilivyo haina maana kutokana na CCM kung’ang’ania kukaa madarakani kwa nguvu.
“Ninajisikia kusalitiwa. Madhumuni ya Mapinduzi haikuwa kuiweka CCM madarakani milele bali kurejesha madaraka kwa wananchi,” alisema.
Alisema aliambiwa kuwa waliofanya mapinduzi (wakiongozwa na Abeid Amani Karume) walitabiri kuwa ipo siku Zanzibar itakuwa na uchaguzi au Serikali ya Umoja wa Kitaifa lakini CCM hawataki.
“Wakati hao waliofanya mapinduzi wakisema hivyo, CCM haikuwepo, ilikuwepo ASP. Hao ASP hawakuwa wakijiaminisha kuwa watakaa madarakani milele,” alisema.
“Wakati tunaadhimisha mapinduzi ya Zanzibar, ni vyema Watanzania wakafahamu kuwa malengo ya mapinduzi hayo yalikuwa ni kuondoa ubaguzi wa aina yoyote na kuweka misingi ya kidemokrasia lakini CCM wamevuruga,” alisema Fatma.
/MWANANCHI.
Wewew dada unaona hizo mali alizotuibia baba yako huyo Maalim ndio atakuja kuzilinda?
ReplyDeleteYaguju!!!
Yanayotokea Bara na Visiwani yatatokea, ngojea kidogo tu!
Tutataifisha mali zote mlizotuibia. Tutakubakishieni nyumba ya Maisara tu ambayo kweli mmerihisi kihalali. Zilizobakia zote pamoja na nyumba iliyokuwa ya watoto wa Forodhani tutazitaifisha pia.
MAJIBU YA WAZI YA MWANASHERIA BIBI FATMA KARUME AMBAE NI MTOTO WA AMANI KARUME.
ReplyDeleteKwanza kabisa sina budi kukushukuru sana kwa weledi wako wa kujitokeza kifua mbele katika masuala yanayosiana na siasa za Zanzibar hivi sasa. Hii inaonesha dhahir kwamba siasa iko kwenye damu yako na unaumwa sana na nchi hii kutokana na historia ya familia yako na Zanzibar.
Naomba kukumbusha tuu dada yangu kwamba unayoyafanya sasa hivi si akili yako. Kwa sisi tunaokujua unatumika na umeamua kutumika kwa faida ya familia yako Fatma.
Kilichotushangaza zaidi ni hii kauli yako ya leo kwenye gazeti la Mwananchi Alkhamis 7Jan 2016. Unapomtaka Dr Shein akae pembeni.
Swali langu kwako na Baba yako mbadala wa Dr Shein akeshaondoka awe nani. Baba Yako Amani Karume???
Ngoja nikukumbushe kumbukumbu kidogo.
Baba yako alikiwa Rais hapa Zanzibar kwa miaka 10. katika miaka hiyo yote ya uongozi wake alifanya mengi mazuri na mengi ya nuni wa firauni. Hatukusikia kupaza sauti yako hata mara moja. au ulikuwa BUBU kipindi kile Fatma????
Ulikuwa wapi wakati Baba yako alipowauwa Wazanzibar wasio na hatia kule Pemba???
Ulikuwa wapi wakati baba yako anaiendesha Serikali kiushemeji shemeji???
Ulikuwa wapi wakati baba yako Rais alipokuwa akipora ardhi za wanyonge tena waliowengi wa Zanzibar akiwa ni pamoja na mjomba wako Mansori na Bibi yako Fatma Karume???.
Hukuwahi wala hukuthubutu kutoa kauli yoyote ile dhidi ya baba yako au Serikali yake. Ulinyamza kimya na kufaidi matunda ya Mapinduzi na Serikali yake.
Fatma dada yangu hakuna asiejua kipindi chote cha Urais wa Baba yako ulikuwa ndio mshauri wake wa karibu wa masuala ya Sheria Zanzibar. Ulikuwa a shadow AG. Baba yako Karume hakiwa akihitajia ushauri kutoka kwa AG wake Marehemu Iddi Pandu Hassan. Alibase zaidi kwako jee kwanini usitumie fursa hiyo kumshauri Baba yako vizuri namna ya kuendesha Serikali????
Washwahili wamesema nyani haoni Kundule. Bi Fatma na Baba yako unakumbuka ulimshauri Rais Karume wakati huo mwezi May 2010 ajiongezee muda wa kukaa madarakani kwa kisingizio cha kusimamia makubaliano ya muwafaka. Draft paper umeandika wewe Fatma na Abubakar wa cuf iliyotaka karume aendelee kuongoza kwa miaka miwili zaidi hadi 2012/2013 ambapo kwenye draft yako ukaweka Baba yako awe Rais na Maalim Seif awe Waziri Kiongozi???? Sisi tuliowengi tunakumbuka hilo Dada yangu na wala hatulisahau.
Shukrani za pekee kwa malaika wema walioweza kulizima ovu lile ulilomshauri Baba yako ili mupaye fursa ya kuzidi kutuangamiza Zanzibar. Maana lengo lenu ni kuitumia ile miaka miwili kusaini mikataba ya mafuta ili muwe na interest security kwenye oil industry.
Mwenyezi Mungu hakuwa nanyi bomu likaripuka. pone pone wewe na baba yako ndio mkatuletea mseto huu uliokuwa nao sasa ambao bado mnaendeleza chokochoko zenu kutokana na kutokuwa tayari kuachia madaraka 2010. Hali hiyo ndio inayowafanya kutompa raha ya kuongoza Dr Shein. kwa kumfanyia kila aina ya vituko. Mna bahati Dr Shein mkimya na mpole angekuwa Komandoo mko jela wote nyie.
..........inaendelea kutoka hapa juu
ReplyDeleteNaomba tujibu Bi Fatma aondoke Dr Shein aje nani Baba yako kutumaliza zaidi au Maalim Seif( a new alliance)
Wakili Fatma wewe sio wa kusema ulikuwa unyamaze kimya lkn ni ngumu kunyamaA kwa binaadamu yoyote maana maslahi uliyokuwa unayapata serikali iliyopita yameyeyuka ghafla. Sasa unaganga njaa kwa kumshupalia Baba wa watu Dr shein ili ujulikane na wewe upo.
Ule wakati wa kudharauliwa AG ukapewa kipaumbele wewe Fatma sasa haupo.
Unakumbuka ulipopewa tenda na Baba yako kusimamia kesi ya Bandari wewe na Mulamula hivi smz ilikulipa kiasi gani??? Kwanini uisimamie wewe ile kesi kwa niaba ya serikali badala ya AG.
Na ile kesi ya Eco Tec vs Ministry of Financd ya Zanzibar???? Zote baba yako alikupa usimamie wewe AG kivuli??? Malipo yako yalikuwa kiasi gani unaweza kutuwekea hadharani???
Ile kesi ya kugonga meli ya bandari iliyokufikisha hadi UK... burungutu lake vipi????
Fatma wewe mbinafsi na mchoyo sana. Na wala hujaelekea kabisa uko selfish kabisa hebu mwachie Dr Shein aendelee na kazi zake dada wewe... Una kijicho cha njaa na ilihal umeshiba...ulipokuwa BP unafanya kazi na ulipohama si uliiba clients wote wa BP na ukahama nao. BP hawakusahau wala hawakusamehe kwa dhambi hiyo.
Bi Fatma kama wewe mjuzi wa sheria kweli naomba nikuulize suala la mwisho. Inajulikana uliwahi kuuwa kwa mwendo kasi wa gari na kumginga mtu wakati unarudi shamba na umelewa chakari, bahati nzuri uliweza kuilaghaibile familia ya kuwalipa kifuta machozi. Kama mwanasheria nguli unahisi umefanyanya sahihi???? jee haki imetendeka hapo???
Bi Fatma mwisho tunakuomba bora tulia udumishe ndoa yako na dr Omar usimtie ila au dosari kaka wa watu. akaonekana kama kapata mke mwehu anapayuka tuu kwenye media. Naamini Omar hana mashaka makubwa kama uliyonayo au unaendeleza fikra za mwanamme wako wa zamani Rashid ulipokuwa nae UK?? mtoto wa Bw Salim Rashid.. amekukoleza uhizbu kidogo??
Tunakuomba sana tuheshimiane Fatma. kama kusoma umesoma wewe sisi wengine hata elimu hatuna lkn tuna maarifa ambayo wewe huna wala baba yako hana.
Na mwisho kabisa na mwisho tunasema kwamba usifanye kukurukakara zozote za kisiasa. hapa tulipofika ukoo wa karume hautawali Zanzibar tena.
tafuta kazi nyengine ukafanye dada.
Ahsante Sana
wako
Mtandao wa wanyonge waliowengi Zanzibar