Halmashauri ya Jiji la Tanga imesalimu amri kwa madiwani wa Ukawa waliokuwa wakipinga uundwaji wa kamati za baraza hilo kwamba zimeundwa kinyemela ambapo Kaimu Mkurugenzi amekubali kusitisha chaguzi za wenyeviti wa kamati hadi hapo taratibu zitakapo kamilika.
Halmashauri hiyo iliunda kamati za baraza hilo ambazo madiwani wa Ukawa walizikataa wakidai zimeundwa kinyume na sheria ya TAMISEMI na kulazimika kuunda tume ya kutaka ufafanuzi kwa Mkurugenzi huyo kwa kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo.
Uchunguzi uliyofanywa na Nipashe ulibaini kuwa siku moja baada ya kaimu mkurugenzi huyo, Dk Wedson Sichalwe kukutana na tume hiyo na kufanya mazungumzo nayo aliandika barua kwa wajumbe kusitisha zoezi la
uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo.
Hali hiyo ilielezwa kama ni ushindi wa tume hiyo ambayo licha ya kupinga kamati hizo lakini pia ilimtaka asimamishe zoezi la chaguzi za wenyeviti wake na kuitisha kikao halali chenye mamlaka kisheria ya kuunda kamati hizo.
Hata hivyo Dk Sichalwe alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na sakata na mkanganyiko wa uundwaji wa kamati hizo, aling’aka na kudai kuwa licha ya kuwa Kaimu Mkurugenzi lakini hana mamlaka ya kuelezea kilichojiri ndani ya kamati hizo kwa kuwa hairuhusiwi kisheria.
“Unajua hata huyo aliyekueleza amekiuka kanuni na anastahili kuchukuliwa hatua, vikao vya kamati hizi ni vikao vya ndani na ni mwiko kwa mtu yeyote kuyatoa nje ya kikao mambo yaliyozungumzwa humo kwa sababu hiyo mimi sina mamlaka kufanya hivyo na mimi nitakuwa nimekiuka” alisema Dk Sichalwe.
Aidha alibainisha kuwa kilichozungumzwa ndani ya kikao hicho kinamanufaa kwa halmashauri,jamii na taifa kwa ujumla na kutoa wito kwa wapenda maendeleo wa Tanga kuvuta subra ili taratibu zinazofanywa ziweze kuleta matunda.
“Mimi nawaomba ndugu zanngu waandishi na wakazi wa Jiji la Tanga kwa ujumla wasiwe na haraka tunachokifanya ni kile chenye manufaa na mustakabali na wananchi wetu na taifa……watuamini tutatekeleza makubaliano yatayotokana na mazungumzo” alisema.
Kwa upande mwingine Dk Sichalwe alikiri kuwepo kwa maandalizi ya kikao kinachodaiwa na madiwani ambacho alibainisha kuwa ndicho chenye mamlaka ya kuunda kamati za mabaraza ya halmashauri hata hivyo hakueleza lini kikao hicho kitakutana na kuondoa utata huo.
Halmashauri ya Jiji la Tanga imeingia kwenye malumbano makubwa siku yalipotangazwa matokeo ya uchaguzi wa meya wa Jiji hilo ambayo msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza mgombea wa CCM, Mhina Mustaph kuwa mshindi kwa kupata kura 19 dhidi ya kura 18 za Rashid Jumbe CUF.
Katika matokeo ya uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka jana, Chama cha Wananchi CUF chini ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA waliibuka ushindi wa ubunge na madiwani katika Kata 15 kati ya 27 zinazounda Jiji la Tanga.
Kwa matokeo hayo katika baraza la halmashauri CUF inawajumbe 20 na Chama cha Mapinduzi CCM kinawajumbe 15 pamoja na wabunge na madiwani viti maalumu waliyopatikana kulingana na idadi ya Kata kilichoshinda
kila chama.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment