.png)
Katika mabadiliko hayo pia Magufuli amemwondoa Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Clodwing Mtweve na kumteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, wateule hao wanakwenda kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.
Tarifa hiyo ilisema Clodwing Mtweve amekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Sefue alisema Chagonja anakwenda Katavi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa pia.
Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Magufuli amewateua Makamishna hao wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.
Makamishna Mtweve, Chagonja na Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa leo Jumamosi asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment