Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 5, 2016

Majaliwa ainyooshea kidole NFRA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) mjini Songea akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameutaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuhakikisha wakulima wa mahindi wanapatiwa magunia ya kuhifadhia mazao yao.
 
Agizo hilo alilitoa jana katika ziara yake ya siku tatu ya kikazi  mkoani Ruvuma na kwamba anatekeleza agizo la Rais John Magufuli kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa njaa.
 
Majaliwa alisema wafanyabiashara wamekuwa wakipatiwa magunia na NFRA kwa ajili ya kununulia mahindi lakini wakulima wanapoomba kupatiwa imekuwa ni tatizo kwao kuyapata kwa urahisi.
 
Alionyesha kusikitishwa na vitendo hivyo vinavyofanywa na wafanyabiashara wajanja, ambao wamekuwa wakipita vijijini kuwarubuni wakulima na kununua mahindi kwa bei ndogo ambayo hailingani na uzalishaji wa zao hilo.
 
Alisema kumekuwa na mianya ya rushwa inayofanywa na wafanyabiashara hao kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa NFRA kwa lengo la kujinufaisha watu wachache huku mkulima wa kawaida akiendelea kuteseka na mazao yake shambani.“Magunia yanayonunuliwa na serikali kwa ajili ya kuhifadhia zao hili, ninazo taarifa za kutosha kwamba hayamfikii mkulima kule kijijini, badala yake yanaishia kwa watu wachache”, alisema Waziri Mkuu.
 
Alisema serikali ina wajibu wa kuhifadhi chakula katika mazingira yanayokubalika ili kisiharibiwe na wadudu waharibifu, hivyo ameitaka NFRA Kanda ya Songea kuhakikisha mahindi yaliyohifadhiwa chini ya ardhi yanatafutiwa sehemu nyingine ili yasiharibike.
 
Alifafanua kuwa uhifadhi wa aina hiyo, usalama wake ni mdogo na kwamba mlundikano huo wa magunia yaliyosheheni mahindi katika hifadhi unasababishwa na wakala kuwa na upungufu mkubwa wa maghala.
 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alihoji kuwepo kwa  msongamano wa malori kandokando ya barabara ya Songea – Mbinga.
 
Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha malalamiko  kutoka kwa wasafirishaji kuwa magari yanayoingia kupakia mahindi, NFRA huwapatia watu wanaojulikana kwanza, ndipo huruhusu wengine kitendo kinachoonyesha kuwepo upendeleo.
 
Awali, Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama, alisema tatizo la soko la mahindi katika mkoa huo ni kubwa, hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano, iangalie namna ya kutafuta masoko ili wakulima wadogo wapate fursa ya kuuza mazao yao.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment