Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 11, 2016

Nahodha: Mapinduzi yalindwe kwa jamii kuelimishwa kujenga uchumi Zanzibar.

Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha.
Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha, amesema Mapinduzi ya Zanzibar hayawezi kulindwa bila ya jamii kupatiwa elimu ya kutosha na kujenga uchumi imara visiwani humu.
 
Nahodha aliyasema hayo alipokuwa akifunga kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi lililofanyika Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana. Alisema misingi ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kubaki imara kama jamii itapatiwa elimu ya kutosha ikiwamo ya ufundi na uzalishaji katika nyanja mbalimbali kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
 
Nahodha alisema Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, aliijenga Zanzibar yenye maisha bora katika huduma za jamii baada ya kufanikiwa kuwekeza katika elimu na sekta ya viwanda na kilimo.
 
Alisema hayati Karume alikuwa kiongozi wa vitendo na siyo nadharia na katika kipindi cha uongozi wake wa miaka minane, alifanya mambo mazito kwa wananchi wake ikiwamo kuwapatia nyumba za makazi na huduma bure za jamii kama maji, matibabu na elimu kabla ya kutokea mabadiliko ya kuchangia huduma hizo.Nahodha alisema iwapo serikali itaimarisha sekta ya elimu na jamii kuwekeza katika eneo hilo, Zanzibar itajenga uchumi imara na kufanikiwa kulinda misingi ya Mapinduzi yake.
 
“Matumaini makubwa ya kupokea mfumo wa vyama vingi vya siasa yalikuwa kuona unasaidia kukuza uchumi, lakini bahati mbaya umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake,” alisema Nahodha.
 
Akijibu hoja za washiriki wa kongamano hilo baada ya kuchangia mada kuhusu mwelekeo na mwenendo wa siasa za dunia katika kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi mstaafu Ali Abeid Karume, alisema Mapinduzi ya Zanzibar yatalindwa na Wazanzibari wenyewe.
 
Alisema pamoja na Zanzibar kuwa na mfumo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), malengo na madhumnuni yake bado kuonekana kutokana na mgawanyiko unaoendelea kujitokeza katika jamii na serikali yenyewe.
 
Alisema lengo kubwa la kuundwa serikali ya pamoja ni kudumisha amani na umoja wa kitaifa kwa wananchi wake badala yake imekuwa ghasia.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment