Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, January 7, 2016

SMZ yaahidi kulinda malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar!

Makamu wa Pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (pichani juu), amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kulinda na kuendeleza malengo ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Alisema mbali na malengo ya Mapinduzi, serikali itaendelea kutekeleza kazi zote zilizokuwa zimeahidiwa na chama cha ASP kabla ya kuungana na TANU na kuzaliwa CCM mwaka 1977.
Balozi Seif alisema hayo jana alipokuwa akihutubia wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji safi katika kisiwa kidogo cha Tumbatu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema serikali inatambua kuwa maji ni uhai na kuwataka wananchi kuchukua hatua za kuhifadhi vyanzo vya maji na kujiepusha na uharibifu wa mazingira visiwani humo
“Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Zanzibar hasa vijijini inatia moyo kutokana na jitihada zinazochuliwa na serikali,” alisema.
Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, takriban watu milioni mbili duniani kote hupoteza maisha kutokana na kutumia maji yasiyo salama na kusababisha kukumbwa na maradhi ya milipuko kama kuhara damu na kipindupindu.
“Watoto wapatao 5,000 hupoteza maisha kila siku duniani kote kutokana na ukosefu wa maji safi na mtu mmoja kati ya 10 duniani hawapati maji safi na salama,” alisema Balozi Seif.
Alisema ugomvi mkubwa unaibuka na kuendelea katika maeneo tofauti nchini kati ya serikali na baadhi ya wananchi kutokana na tabia ya watu wachache kuamua kujenga nyumba za makazi katika vianzio vya maji.
Upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa  Zanzibar,  Ali Khalil Mirza, alisema mradi huo unatarajia kuhudumia wananchi 8,252 wa kisiwa hicho. 
Mirza alisema mradi huo utakaogharimu Sh. bilioni moja, utasaidia kuondoa tatizo la muda mrefu la maji kwa wananchi waliokuwa wakilazimika kuvuka bahari kusaka maji nje ya kisiwa hicho.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment