Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 11, 2016

Takukuru yawaburuza vigogo mahakamani Geita



Mwananchi
Geita. Aliyekuwa mweka hazina wa Halmashauri ya Geita Victor Swai, mlipa fedha (keshia) Sundi Makonda na Ofisa mipango wa Halamshauri hiyo James Masolo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wa Geita na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  (TAKUKURU) wakikabiliwa na makosa mawili tofauti likiwemo la wizi wa zaidi ya Sh31milioni.
Mwanasheria wa TAKUKURU mkoani hapa, Osborn Pais akisaidiana na Augustino Mtaki alidai mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Safina  Simfukwe kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa mawili likiwemo la wizi wa zaidi ya Sh31milioni.
Pais alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda
kosa la kuiba fedha za halmashauri hiyo mnamo Oktoba 21 mwaka 2010
kinyume cha kifungu cha sheria 258 na kifungu cha 270 ya kanuni za
adhabu sura ya 16 iliyorejelewa mwaka 2002.
Mwanasheria wa Takukuru aliieleza mahakama hiyo kuwa kosa la pili
linalowakabili watuhumiwa hao kwa pamoja ni kumsababishia mwajiri
hasara ya zaidi ya Sh31milioni.
Alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa  kinyume cha
sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 iliyorejelewa 2002 aya ya 10 aya ndogo ya kwanza kifungu cha 57 (1) na kifungu cha 60 (2) cha sheria ya uhujumu uchumi .
Watuhumiwa hao kwa pamoja walikana kutenda makosa hayo ambapo Hakimu
wa mahakama hiyo Safina Simfukwe aliwaeleza kuwa kuwa dhamana iko wazi
kwa mujibu wa sheria na kuwataka kila mmoja kulipa nusu ya fedha wanazotuhumiwa nazo au kuweka dhamana ya mali yenye thamani hiyo
pamoja na kuwa na wadhamini wawili wenye mali au nusu ya  fedha
wanazotuhumiwa nazo.
Watuhumiwa wote walikidhi vigezo vya dhamana ambapo kesi hiyo
imeahirishwa hadi Februari 11 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya
kusikiliza hoja za awali.

No comments :

Post a Comment