NAIBU Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wiliam Ole Nasha, ametoa siku saba kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, kuhakikisha wanatatua migogoro iliyopo kati ya wakulima na wafugaji.
Pamoja na hali hiyo wamewataka watendaji hao kuepuka vitendo vya rushwa, ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa kila mmoja.
Naibu waziri alisema hayo juzi katika ziara yake ya siku moja yenye lengo la kutatua migogoro iliyopo kati ya wakulima na wafuga, ili kuimarisha usalama wa raia nchini.
Akiwa katika Kijiji cha Mtanange wilayani humo, Ole Nasha, alisema Serikali inahitaji kuhakikisha migogoro iliyopo inatatuliwa, ili watu waishi kwa amani bila usumbufu wowote.
“Serikali ya awamu ya tano inahitaji kufanya kazi kwa kuhakikisha kwamba kero zilizopo zinatatuliwa kwa wakati, masuala ya wakulima na wafugaji tunayapa kipaumbele ili kuimarisha usalama wa raia.
“Pia nawaomba msikubali kuingiza masuala ya ukabila sisi sote ni Watanzania kila mmoja wetu ana haki ya kuishi mahali popote ilimradi afuate sheria zilizopo,” alisema.
No comments :
Post a Comment