Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 11, 2016

Waziri: Siko tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa idara, taasisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, amesema hayuko tayari kufukuzwa kazi kutokana na uzembe wa idara au taasisi yoyote iliyoko chini yake.
 
Waziri Ktwanga anafanya ziara katika idara mbalimbali anazoziongoza, aliyasema hayo baada ya kufika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam na kukutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa jeshi hilo.
 
Alisema hatakubali kuona anawajibishwa na Rais John Magufuli, kwa sababu ya uzembe wa idara yoyote iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, hivyo atawawajibisha watendaji wazembe kabla hajawajibishwa yeye.
 
Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga alilitaka jeshi hilo kuimarisha ukaguzi katika majengo marefu na mafupi ikiwamo vyombo vya usafiri na usafirishaji.
 
Alisema Jeshi la Zimamoto linapaswa kusimamia sheria ya uokoaji inayowataka wananchi kupisha magari ya Zimamoto pamoja na gari la wagonjwa pindi yanapokuwa katika dharura.“Si mnafahamu sheria ya uokoaji inavyosema, hata msafara wa Rais unapaswa kupisha gari za Zimamoto au la wagonjwa linapokuwa katika dharura. Iweje wananchi wasipishe gari la Zimamoto? Nataka msimamie sheria,” alisema Kitwanga.
 
Aliongeza kuwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapaswa kuhakikisha kunakuwapo na usalama wa mali na uhai wa wananchi kipindi chote kunapotokea janga la moto pamoja na kwenda na wakati kwa kuwa na vifaa vya kisasa kwa sababu nyakati hizi miji imekuwa inajengwa majengo marefu.
 
Alisema mtu yeyote anayefanya kosa achukuliwe sheria kali kwa kupigwa faini na kwamba gari la Zimamoto halipaswi kusubiri njiani au kulipisha gari lingine linapokuwa kazini.
 
Naye Kamishna Jenerali Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mhandisi Pius Nyambacha, alisema jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kutendea kazi.
 
Nyambacha alisema thamani ya vifaa vya kuzimia moto vinavyohitajika vinafikia Sh.bilioni moja.
 
Alisema pia jeshi hilo linakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi ambapo kwa sasa lina askari 2,357 malengo makuu yakiwa ni kuwa na askari 4,500.
 
Vile vile, Nyambacha alisema jeshi hilo lina uhaba wa visima vya kujazia maji na halijapewa fedha za maendeleo kutoka serikalini kwa miaka mitano sasa, jambo linalowakwamisha katika utekelezaji wa malengo waliyojiwekea.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment