
Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Uwanja wa ndani wa Makao Mkuu ya CCM Kisiwanduwi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Alisema Uchaguzi Mkuu wa marudio Zanzibar hakuitishwa na CCM, CUF au Chadema, bali Tume ya Uchaguzi ndiyo walioitisha baada ya kujiridhisha kuwa Uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ulikuwa na kasoro.
Alisema mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec)ndiyo yenye mamlaka ya kuratibu na kusimamia uchaguzi Zanzibar.
“CCM tumeshakubali kushiriki uchaguzi wa marudio na suala la kushiriki au kutokushiriki ni jambo la hiyari katika demokrasia,”alisema Dk. Shein.
Alisema uchaguzi wa Zanzibar umelazimika kurudiwa ili kukidhi matakwa ya demokrasia na kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kukamilisha haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Alisema uchaguzi wa Zanzibar umelazimika kurudiwa ili kukidhi matakwa ya demokrasia na kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kukamilisha haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha, Dk. Shein aliwataka wananchi kudumisha na kuimarisha amani ya Zanzibar lakini alionya serikali haitofumbia mtu yeyote ambaye atajaribu kuvuruga amani na mshikamano kwa wananchi wake.
Alisema vyombo vya dola vipo makini kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarishwa na kuwataka wananchi kuendeleza utamaduni wa Zanzibar wa kuiishi katika mazingira ya amani kwa manufaa ya Zanzibar na watu wake.
Alisema kurejewa kwa uchaguzi Zanzibar isiwe sababu ya kuchafua amani ya nchi na kuonya kuwa kwa mwenye ubavu ajaribu kufanya na kwamba atakiona cha moto.
Dk. Shein alisema uchaguzi utafanyika kwa amani na salama na kwamba sio kweli kama kutakuwa na sitofahamu kama inavyodaiwa na watu na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Upande wake mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema wana-CCM wasibabaike na kauli ya CUF ya kutoshiriki uchaguzi wa marudio wa Machi 20, mwaka huu.
Alisema kuwa inawezekana ikawa uongo wao wa kisiasa wa kujaribu kudanganya wananchi na kwamba wakishiriki sawa na wasiposhiriki ni sawa .
“Serikali itahakikisha inaimarisha ulinzi siku ya uchaguzi ili wanaoenda kupigakura wasibughuziwe.”alisema Balozi Seif.
Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana, alisema CCM imejipanga kimkakatina kuhakikisha inashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Upande wake naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema upo ushahidi wa Uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana kuhujumiwa lakini jambo la kushangaa hakuna aliyefikishwa katika vyombo vya sheria kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali ya Zanzibar
“Hatutaki kuingilia uhuru wa mahakama lakini tunataka wakipelekwa mahakamani mahakama zitende haki kwa mujibu wa sheria,”alisema Vuai.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment