Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 5, 2016

Kitendawili Mwenyekiti PAC kutenguliwa leo, mawaziri vivuli hadharani.

Image result for MBOWE


Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Kambi ya Rasmi ya Upinzani na Bunge, Uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Hesabu za Serikali (PAC), na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), unatarajiwa kufanyika leo sambamba na kutangazwa kwa Baraza Kivuli la Upinzani Bungeni.

Baraza hilo linalotarajiwa kuundwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, litachuana na lile la Rais John Magufuli.
 
Taarifa ambazo gazeti hili imezipata, hatua hiyo ni matokeo ya kikao kilichofanyika juzi kati ya ofisi ya spika na ile ya kambi ya upinzani.
 
Katika kikao hicho pamoja na watu wengine, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mbowe walikubaliana kutekeleza mambo hayo mawili leo.
 
“Mbowe alisema baraza hilo atalitangaza mapema kesho (leo) na kwamba watafanya uchaguzi kwenye kamati hizo mbili ambazo hawakufanya uchaguzi,” alisema.
 
Katika baraza hilo, linadawai kuwa na muundo sawa na Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya tano ambalo lina wizara 19.
 
Aidha, inasemekana katika baraza hilo, atakuwapo Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalengo, Zitto Kabwe.Baraza hilo pia litazingatia uzoefu na taaluma za wabunge pamoja na kuangalia muundo wa muungano.
 
Hata hivyo, Nipashe lilimtafuta Mbowe kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi zaidi lakini namba yake ilikuwa inaita bila kupokelewa.
Hivi karibu Nipashe lilielezwa kuwa, kutakuwa na mabadiliko madogo kwenye baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge.
 
Katika mabadiliko hayo, ni pamoja na Zitto aliyekuwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Jamii, sasa atapelekwa ile ya Hesabu za Serikali (PAC).
 
Pia Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa wakati wa Bunge la 10.
 
“Mbali na kambi ya upinzani bungeni, kulikuwa pia na shinikizo la mataifa ya nje ambayo yanataka hizi kamati za kuangalia serikali ziongozwe na upinzani, jambo ambalo spika pia alikuwa anataka lakini kwa sababu fulanifulani ikawa kama ambavyo tuliona kamati zimepangwa awali,” kilisema chanzo chetu cha habari.
 
Spika wa Bunge, alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo, hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.
Naibu Katibu wa Bunge, John Joel, alipotafutwa, alisema suala hilo halijafika mezani kwake bado.
 
“Kwa kweli siwezi kusema chochote kwa sababu hilo bado halijanifikia, lakini kama hayo mabadiliko yamefanywa ama yatafanywa na spika ni sawa kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka kikanuni.
 
"Kwa sababu kulikuwa na baadhi ya wabunge wanaomba kuhamishwa kwenye kamati na sisi tulichokuwa tunafanya ni kupeleka kwa spika kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwabadilisha,” alisema Joel.
 
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilah, alisema bado hajapata taarifa ya suala hilo na kutaka aulizwe spika mwenyewe.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment