Deus Bugaywa
Toleo la 446
Wapo wanaaomiani kwamba siku mia ni chache sana kuweza kutoa picha au mwelekeo wowote wa maana wa jinsi awamu hii itakavyoendesha mambo yake.
Lakini wapo pia wanaoamini kwamba siku hizo zinatosha kutupa mwelekeo na nini cha kutarajia kutoka katika serikali hii ya Rais John Magufuli.
Mjadala kuhusu muda ni muhimu sana kwa sababu ni moja wa rasilimali adhimu ambazo huwezi kuizalisha mara mbili au zaidi (reproduce), kwamba muda ukipotea hiyo ni hasara isiyofidiwa, kwa hivyo vyovyote vile iwavyo muda katika kufanya kila jambo kwa mafanikio ni muhimu sana, ikiwemo katika utekelezaji wa ahadi ya mbadiliko ya kweli kwa Watanzania na ujenzi wa Tanzania mpya kama Rais alivyoahidi wakati wa kampeni.Na pengine ni muhimu wakati tunahesabu muda katika muktadha wa utawala wa kisiasa na uongozi, tukaazima hekima ya mtunga Zaburi kwamba, “Maana miaka elfu machoni pako (Munguy) ni kama siku ya jana ikiisha kupita, na kama kesha la usiku.”
Hakuna anayeweza kuibua mjadala juu ya ukweli kwamba nchi inazizima, taifa linaoja radha mpya ya uongozi uliokuwa umeanza kusahaulika, vyeo sasa vimeanza kuwaogopesha watu, uteuzi sasa siyo jambo la kupongezana na bila saka hata vichwa vya habari vya magazeti yetu haviwezi tena kuuita uteuzi wowote ule ‘ulaji’.
Sasa majipu yanatumbuliwa tena bila ganzi. Walau siku mia za mwanzo za Serikali ya Awamu ya Tano zinatupa picha ya wazi ya dhamira yake ya kurejesha taifa katika hali ya kawaida, yaani watu watimize wajibu wao, wale kwa jasho, watumishi watumike kwa haki, wafanyabiashara wafanye biashara yao kwa misingi ya biashara inayopaswa, walipe kodi na wasiingize bidhaa feki au zilizo chini ya kiwango.
Hapa ndipo tulipo, kile kinachofanywa na serikali ya Magufuli ni kuturejesha mahali tunapopaswa kuanzia safari ya maendeleo, safari yenyewe hatujaianza.
Ni kweli kazi inayofanyika sasa ni muhimu na inapaswa kufanyika ili kurejesha nidhamu iliyokuwa imepotea katika jamii yetu. Kazi hii siyo nyepesi hata kidogo ndiyo maana Rais Magufuli na wasaidizi wake wamekuwa wakiomba kila mara Watanzania wawaombee katika kazi waliyojipa ya kutumbua majipu. Lakini kazi iliyoko mbele yao baada ya utumbuzi wa majipu ni ngumu zaidi, hii itahitaji zaidi ya maombi na ushirikiano. Msanifu wa Taifa la Singapore (The architecture of Singapore) Lee Kuan Yew, wakati anaijenga upya nchi hiyo kutoka katika mazoea ya rushwa na ufisadi kama tulivyo sisi alisema.
“It is easy to start off with high moral standards, strong convictions, and determination to beat down corruption. But it is difficult to live up to these good intentions unless the leaders are strong and determined enough to deal with all transgressors, and without exceptions. CPIB (PCCB in our case) officers must be supported without fear or favor to enforce the rules.” Conviction
Kwa tafsiri isiyo rasmi Yew anasema, “NI rahisi kuanza na kiwango cha juu cha uadilifu, kwa kujiamini na dhamira ya dhati kutokomeza rushwa. Lakini ni vigumu kuiishi dhamira hii njema isipokuwa kama una viongozi wenye nguvu na dhamira isiyoteteleka kushughulikia wakosaji wote bila suluhu. Maafisa wa CPIB (Taasisi ya kupambana na rushwa Singapore) ni lazima waungwe mkono bila woga wala upendeleo kusimamia sheria.”
Anachokisema kiongozi huyu mahiri ni kujenga mfumo imara wa kupambana na rushwa, kwamba suala hili halipaswi kuishia kwenye dhamira safi ya Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu, vita dhidi ya rushwa inapaswa kuwa kwenye mfuo wetu wa utawala. U – dhati wa dhamira hiyo unapswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya taasisi zetu. Na hili ni gumu zaidi lakini kama ni lazima tuifikishe nchi hii kwenye hadhi ya uchumi wa kati au hata kuwa ‘donor country’ kama anavyosema Rais Magufuli, hatuna hiyari nalo, ni suala lisiloepukika, ni lazima tulitekeleze.
Magufuli na timu yake hawapaswi kurudia makosa ya awamu ya kwanza, ni lazima pia kama kizazi kipya cha Taifa hili, tujifunze kwa makosa ya watangulizi wetu. Pamoja na dhamira njema ya Baba wa Taifa kujenga Taifa la Ujamaa na kujitegemea, pamoja na nia safi ya kuanzisha Azimio la Arusha, lililoweka misingi ya utu, usawa, uwezo wa kujitegemea, maadili ya viongozi na miiko yake, wema wote huo ulikuwa kwenye moyo na akili ya Mwalimu Nyerere peke yake, na watu wengine wachache waliomwelewa na kumwamini.
Wengine wengi ni kama walikuwa wanasubiri tu aondoke madarakani ili wafanye yao, ndiyo maana ilichukua chini ya muongo mmoja kuvunja vunja misingi ya Azimio la Arusha iliyojengwa kwa takribani miaka 30. Wasiolitakia mema taifa hili walikutana kimya kimya wakalifutilia mbali (wenyewe wanasema walilizimua) azimio hilo ambalo liliweka misingi imara ya uongozi, tunayoililia leo.
Kilio cha Mwalimu mpaka anakutana na mauti kwamba anajaribu kila mara kusoma kijitabu cha Azimio la Arusha, lakini hajaona wapi azimio hilo lilikuwa na tatizo. Lakini baadaye tukiamua kuyatazama mambo kwa uhalisia wake tutaona kuwa tatizo halikuwa azimio hilo wala misingi yake, tatizo lilikuwa ni shingo ngumu na ugumu wa mioyo wa waliokuwa na jukumu la kusimamia misingi yake.
Anachokifanya Rais Magufuli leo, ni juhudi za kufufua Azimio la Arusha, walau katika sura tofauti, lakini misingi ni ile ile, anasisitiza uadilifu wa viongozi na nidhamu kwa utumishi wa umma, anasimamia misingi ya kujitegemea, anataka wananchi wapate huduma za jamii elimu, afya na nyinginezo kwa uhakika bila kubahatisha, na anapambana na rushwa bila mzaha kwa kuwa ni adui wa haki, anataka cheo kiwe dhamana kweli ya utumishi siyo mradi wa kulimbikiza ukwasi. Haya yote ndiyo yaliunda misingi ya Azimio la Arusha.
Kuyarejesha haya ni kazi ngumu kama anavyokiri Yew, lakini kukiwa na ‘uendawzimu’ kama wa kulizungumzia Azimio la Arusha hadharani, chambilecho Mwalimu, hilo linawezekana. Dhamira hiyo ikitafsiriwa katika mifumo yote ya utawala, kutatuepusha na balaa la kuwa tunaanza upya kila siku, kwamba pamoja na kuwa na awamu ya tano, lakini Rais Magufuli anaonekana kama ndiyo kwanza anaanza upya kulijenga taifa hili.

Muhimu kwetu siyo siku mia au hata elfu, lakini zaidi sana ni kitu gani kimefanyika katika muda huo na nini tafasiri yake kuhusu mwelekeo wetu kama taifa, kilichofanyika kinatoa ishara gani na mwelekeo upi wa huko tuendako, kwa sababu hatuwezi kuukana ukweli wa maisha kwamba tunatarajia uwepo wa kesho kwa sababu kuna leo. Vivyo hivyo uongozi wa Rais Magufuli tutautumainia kutupeleka unakotaka kutupeleka kwa kuangalia nini kinafanywa leo na Serikali yake.
Hakuna anayeweza kuibua mjadala juu ya ukweli kwamba nchi inazizima, taifa linaoja radha mpya ya uongozi uliokuwa umeanza kusahaulika, vyeo sasa vimeanza kuwaogopesha watu, uteuzi sasa siyo jambo la kupongezana na bila saka hata vichwa vya habari vya magazeti yetu haviwezi tena kuuita uteuzi wowote ule ‘ulaji’.
Halikuwa jambo la kustaajabisha kabisa (ingawa katika hali halisi linastaajabisha) miongoni mwa Watanzania hata wahariri, kwamba mtu akiteuliwa Waziri, Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya, anakuwa amepewa ulaji. Ilikuwa kawaida kusoma kichwa kikubwa cha habari, “Fulani aula”, kisa amepewa dhamana ya kutumikia Watanzania.
Kulikuwa na uozo wa jamii nzima kuwaelekeza wateule, waliopaswa kuwa watumishi, kujiona kwamba wamepata nafasi ya kula, na katika hili hawakufanya makosa, walikula kweli mpaka wakaota majipu kila pahala.
Sasa majipu yanatumbuliwa tena bila ganzi. Walau siku mia za mwanzo za Serikali ya Awamu ya Tano zinatupa picha ya wazi ya dhamira yake ya kurejesha taifa katika hali ya kawaida, yaani watu watimize wajibu wao, wale kwa jasho, watumishi watumike kwa haki, wafanyabiashara wafanye biashara yao kwa misingi ya biashara inayopaswa, walipe kodi na wasiingize bidhaa feki au zilizo chini ya kiwango.
Hapa ndipo tulipo, kile kinachofanywa na serikali ya Magufuli ni kuturejesha mahali tunapopaswa kuanzia safari ya maendeleo, safari yenyewe hatujaianza.
Tulipo sasa ni kama mtu aliyetaka kuanza safari yake na reli ya kati kutoka Stesheni ya Mwanza kuelekea Dar es Salaam, lakini mtu huyu akakosea maelekezo ya safari akapanda meli kwenda Bukoba.
Kinachofanyika sasa ni kututoa Bukoba kutuleta Mwanza ili tunaze safari. Safari yenyewe hatujaianza.
Siku hizi mia zimeonyesha dhamira hiyo ya kupambana na uonzo uliokuwepo kila mahali, na kutumbuliwa kwa majipu, lakini ni vyema pia tukautambua ukweli kuwa majipu haya yana chanzo chake, ili tujihakikishie kutokuwa nayo mengine ni lazima kazi ya kuyatumbua yaliyopo iende bega kwa bega na kuweka kinga ya kutopata mengine, ili haya yanayotubuliwa vidonda vyake vikipona tusipate maambukizi mengine, lazima tujenge mfumo imara wa kinga.
Siku hizi mia zimeonyesha dhamira hiyo ya kupambana na uonzo uliokuwepo kila mahali, na kutumbuliwa kwa majipu, lakini ni vyema pia tukautambua ukweli kuwa majipu haya yana chanzo chake, ili tujihakikishie kutokuwa nayo mengine ni lazima kazi ya kuyatumbua yaliyopo iende bega kwa bega na kuweka kinga ya kutopata mengine, ili haya yanayotubuliwa vidonda vyake vikipona tusipate maambukizi mengine, lazima tujenge mfumo imara wa kinga.
Ni kweli kazi inayofanyika sasa ni muhimu na inapaswa kufanyika ili kurejesha nidhamu iliyokuwa imepotea katika jamii yetu. Kazi hii siyo nyepesi hata kidogo ndiyo maana Rais Magufuli na wasaidizi wake wamekuwa wakiomba kila mara Watanzania wawaombee katika kazi waliyojipa ya kutumbua majipu. Lakini kazi iliyoko mbele yao baada ya utumbuzi wa majipu ni ngumu zaidi, hii itahitaji zaidi ya maombi na ushirikiano. Msanifu wa Taifa la Singapore (The architecture of Singapore) Lee Kuan Yew, wakati anaijenga upya nchi hiyo kutoka katika mazoea ya rushwa na ufisadi kama tulivyo sisi alisema.
“It is easy to start off with high moral standards, strong convictions, and determination to beat down corruption. But it is difficult to live up to these good intentions unless the leaders are strong and determined enough to deal with all transgressors, and without exceptions. CPIB (PCCB in our case) officers must be supported without fear or favor to enforce the rules.” Conviction
Kwa tafsiri isiyo rasmi Yew anasema, “NI rahisi kuanza na kiwango cha juu cha uadilifu, kwa kujiamini na dhamira ya dhati kutokomeza rushwa. Lakini ni vigumu kuiishi dhamira hii njema isipokuwa kama una viongozi wenye nguvu na dhamira isiyoteteleka kushughulikia wakosaji wote bila suluhu. Maafisa wa CPIB (Taasisi ya kupambana na rushwa Singapore) ni lazima waungwe mkono bila woga wala upendeleo kusimamia sheria.”
Anachokisema kiongozi huyu mahiri ni kujenga mfumo imara wa kupambana na rushwa, kwamba suala hili halipaswi kuishia kwenye dhamira safi ya Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu, vita dhidi ya rushwa inapaswa kuwa kwenye mfuo wetu wa utawala. U – dhati wa dhamira hiyo unapswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya taasisi zetu. Na hili ni gumu zaidi lakini kama ni lazima tuifikishe nchi hii kwenye hadhi ya uchumi wa kati au hata kuwa ‘donor country’ kama anavyosema Rais Magufuli, hatuna hiyari nalo, ni suala lisiloepukika, ni lazima tulitekeleze.
Magufuli na timu yake hawapaswi kurudia makosa ya awamu ya kwanza, ni lazima pia kama kizazi kipya cha Taifa hili, tujifunze kwa makosa ya watangulizi wetu. Pamoja na dhamira njema ya Baba wa Taifa kujenga Taifa la Ujamaa na kujitegemea, pamoja na nia safi ya kuanzisha Azimio la Arusha, lililoweka misingi ya utu, usawa, uwezo wa kujitegemea, maadili ya viongozi na miiko yake, wema wote huo ulikuwa kwenye moyo na akili ya Mwalimu Nyerere peke yake, na watu wengine wachache waliomwelewa na kumwamini.
Wengine wengi ni kama walikuwa wanasubiri tu aondoke madarakani ili wafanye yao, ndiyo maana ilichukua chini ya muongo mmoja kuvunja vunja misingi ya Azimio la Arusha iliyojengwa kwa takribani miaka 30. Wasiolitakia mema taifa hili walikutana kimya kimya wakalifutilia mbali (wenyewe wanasema walilizimua) azimio hilo ambalo liliweka misingi imara ya uongozi, tunayoililia leo.
Kilio cha Mwalimu mpaka anakutana na mauti kwamba anajaribu kila mara kusoma kijitabu cha Azimio la Arusha, lakini hajaona wapi azimio hilo lilikuwa na tatizo. Lakini baadaye tukiamua kuyatazama mambo kwa uhalisia wake tutaona kuwa tatizo halikuwa azimio hilo wala misingi yake, tatizo lilikuwa ni shingo ngumu na ugumu wa mioyo wa waliokuwa na jukumu la kusimamia misingi yake.
Anachokifanya Rais Magufuli leo, ni juhudi za kufufua Azimio la Arusha, walau katika sura tofauti, lakini misingi ni ile ile, anasisitiza uadilifu wa viongozi na nidhamu kwa utumishi wa umma, anasimamia misingi ya kujitegemea, anataka wananchi wapate huduma za jamii elimu, afya na nyinginezo kwa uhakika bila kubahatisha, na anapambana na rushwa bila mzaha kwa kuwa ni adui wa haki, anataka cheo kiwe dhamana kweli ya utumishi siyo mradi wa kulimbikiza ukwasi. Haya yote ndiyo yaliunda misingi ya Azimio la Arusha.
Kuyarejesha haya ni kazi ngumu kama anavyokiri Yew, lakini kukiwa na ‘uendawzimu’ kama wa kulizungumzia Azimio la Arusha hadharani, chambilecho Mwalimu, hilo linawezekana. Dhamira hiyo ikitafsiriwa katika mifumo yote ya utawala, kutatuepusha na balaa la kuwa tunaanza upya kila siku, kwamba pamoja na kuwa na awamu ya tano, lakini Rais Magufuli anaonekana kama ndiyo kwanza anaanza upya kulijenga taifa hili.
Hii lazima iishie hapa, awamu ya sita ije ijenge juu ya misingi iliyowekwa na awamu ya tano, tusiruhusu tena awamu ya kutengeneza majipu halafu awamu ya saba au nane tena ije ianze kutumbua, hapana, tunahitaji kusonga mbele. Uwezekano huo hata hivyo unategemea sana na kwa kiwango kikubwa wananchi, Bunge na Mahakama ziko tayari kiasi gani kuunga mkono hilo.
- See more at: http://raiamwema.co.tz/kutumbua-majipu-si-kazi-kazi-ni-kuzuia-mapya-yasiote#sthash.Pas2v0kv.dpuf

No comments :
Post a Comment