- Sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM zafana.
- JK aandika historia muhimu ya maisha yake.
- Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweka wazi kwa watumishi wa serikali kutambua kuwa ilani inayotekelezwa ni ya CCM
- CCM mkoa wa Singida watoa madawati 1000 kwa shule za manispaa ya Singida
- Kinana asema CCM inamuunga mkono Rais John Pombe Magufuli na kauli mbiu yake ya hapa kazi tu.
Vijana wa Chipukizi wa CCM wakishangilia miaka 39 ya kuzaliwa kwenye uwanja wa Namfua
Umati wa wakazi wa Singida mjini wakishangilia kilele cha miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwenye uwanja wa Namfua.
Umati wa wakazi wa Singida waliofurika kusherehekea maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa mkoa wa Singida kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mkoa wa Singida kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwenye uwanja wa Namfua.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa mkoa wa Singida ambapo ameandika historia kwenye maisha yake kwani alianza kazi mkoa huo mnamo tarehe 2 aprili,1975 akiwa Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Singida.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yaliofanyika kitaifa mkoani Singida kwenye uwanja wa Namfua.
Yamoto Band wakiburudisha wapenzi na wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akishangilia burudani ya Yamoto Band pamoja na wabunge wa viti mkoani humo Mhe. Martha Mlata (kulia) na Mhe. Aysa-Rose Matembe kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM
Wasanii wa Bendi ya TOT wakishambulia jukwaa huku gitaa likipigwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yaliofanyika kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida.
No comments :
Post a Comment