Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 9, 2016

Muhongo: Wawekezaji ruksa kuuza umeme

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
By Habel Chidawali,Mwananchi 
Mtera. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limefungua milango kwa wawekezaji kuuza umeme moja kwa moja kwa wananchi.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alitoa kauli hiyo jana kwenye kikao cha mameneja na watendaji wa Tanesco kilichowashirikisha wawekezaji wadogo nchini katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera.
“Tumeamua kuondoa urasimu, katika kipindi cha muda mrefu hawa jamaa (Tanesco) wamekuwa peke yao, sasa kuna mambo yanakosekana, lazima tutoe nafasi. Kama mtu anaweza kuzalisha umeme na kuuza tumpe nafasi hiyo,” alisema Muhongo.
Waziri Muhongo alisema kiasi cha umeme kinachozalishwa nchini ni kidogo ikilinganisha na mpango wa Serikali wa kuanzisha viwanda.
Alitaja mahitaji ya umeme kuwa ni Megawati 10,000 hadi 15,000, lakini uliopo sasa hauzidi Megawati 1,500.
Mkurugenzi wa Tanesco, Felschemi Mramba alisema shirika hilo limefungua milango nchi nzima kwa watu wanaotaka kuwekeza na wako tayari kuwasaidia wawekezaji wadogo ili kufikia ndoto zao.
Alisema wawekezaji watakaoshindwa kufuata taratibu Serikali haitawasaidia kwa jambo lolote.
Moja wa wawekezaji, Godfrey Augustine alisema kama urasimu wa uwekezaji ndani ya Tanesco utaondolewa, yako maeneo mengi watu wanaweza kufanikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa bei nafuu.
Augustine ambaye pia ni msimamizi wa mradi wa uwekezaji wa Kanisa kutoka Iyovu, alisema vyanzo vya kupata umeme bila ya kutegemea maji au mafuta, vipo vingi tatizo ni mitaji na urasimu uliopo kwa baadhi ya watendaji.     

No comments :

Post a Comment