Dar es Salaam. Wamiliki wa nyumba sita zilizobomolewa katika eneo la Kijiji Sanaa, Shekilango wamedai kuwa hawajetendewa haki kwani nyumba zao zilikuwa mbali na eneo linalostahili kubomolewa.
Februari 4, saa tatu asubuhi Kampuni ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers iliendesha ubomoaji huo, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya watu waliojenga nyumba katika kiwanja M/S Cool Makers Limited kuondoka.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana walisema wamestushwa na ubomoaji huo ulivyoendeshwa kinyume na taratibu.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mambi Yusuph alisema wao hawaguswi na mgogoro wa ardhi uliopo katika eneo kati ya M/S Cool Makers Limited (mdai), Jumuiya ya Wazazi ya CCM na John Ondoro, kwani kuna umbali kati ya nyumba zao na eneo linalogombaniwa.
“Nimesikitishwa na kitendo hiki, kimekuwa cha ghafla yaani wamebandika tangazo usiku asubuhi wameleta matingatinga yaje kutubomolea hii siyo haki kabisa,” alisema Yusuph huku akionyesha vielelezo halali kama mmiliki wa eneo analilojenga nyumba yake iliyobomolewa.

Mjumbe wa eneo hilo, Baruan Ngwao alisema watakwenda ngazi za juu ikiwamo Manispaa ya Kinondoni, kuonana na mkuu wa wilaya au meya ili kushughulikia tatizo hilo.
No comments :
Post a Comment