
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe.Jecha Salim Jecha imesema kuwa madaftari ya wapiga kura yatakuwa nje ya vituo yatabandikwa wiki moja kabla ya uchaguzi ili kuwapa nafasi wapiga kura kuelewa vituo walivyopangiwa.
Ameyataja matayarisho mengine yaliyokuwa katika hatua nzuri kuwa ni pamoja uteuzi wa wasimamizi wa Majimbo, upangaji wa vifaa na vituo, pamoja na mafunzo kwa watendaji.
Mhe.Jecha ameongeza pia matayarisho ya awali ya uchapishaji wa karatasi za kura yamekamilika baada ya tume kumpitisha mchapishaji wa karatasi hizo na zinatarajiwa kuwasili nchini mwanzoni mwa mwezi wa Marchi.
Akizungumzia mawasiliano kwa vyama vya siasa na wagombea Mhe.Jecha amesema kuwa tume itaendelea kuwahesabu wagombea wote wa uchaguzi uliopita ni halali kutokana na kutofuata utaratibu wa kisheria za kujitoa kwa wagombea.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi nambari 11 ya mwaka 1984 sura ya tatu kifungu cha 31 hadi 37a kinatoa sharti la kuwepo wadhamini wa wagombea na hakuna Chama kilichoiandikia tume kuwa kimefuta udhamini wa wagombea wake kushiriki katika uchaguzi huo.
/ZanziNews.

No comments :
Post a Comment