Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 26, 2016

Dk Shein Amuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Leo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Said Hassan Said.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akiwasili katika Ikulu ya Zanzibar tayari kwa hafla kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Ikulu Zanzibar leo 26-3-2016.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa wakiingia katika Ukumbi wa Ikulu kwa ajili ya hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar leo asubuhi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar Mhe Burhan Sadaat na Balozi Mohammed Ramia wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said Ikulu Zanzibar leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis (katikati) kushoto Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe. Khatib Abrahaman Khati wakihudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said,akipitia hati ya kiapo kabla ya kuaza kwa hafla hiyo Ikulu leo.
Mkurugenzi wa Mashtaka  Zanzibar Nd,Ibrahim Mzee na Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar George Kazi ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu Mjini Unguja
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar Ndg Asaa, akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa wakati wa hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Zanzibar. 
Familia ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Ikulu wakati wa hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.Ikulu leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Ukumbi wa Ikulu kwa ajili ya hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar baada ya kumtangaza jana Mhe Said Hassan Said, Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said Ikulu Zanzibar leo asubuhi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said Ikulu Zanzibar leo kushoto Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee.Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said, akila kiapo Ikulu leo Zanzibar.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya Kiapo ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar baada ya kumuapisha Ikulu leo Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akitia saini hati yake ya Kiapo baada ya kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. Ikulu leo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said baada ya kumuapisha leo Ikulu Zanzibar. 
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar akipongezwa na Mtoto wake baada ya kuapishwa leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said, na familia yake baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Dini waliohudhuria hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu akibadilisha mawazo na Mwenasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said baada ya kuapishwa leo Ikulu Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Afisi ya Rais Ikulu Zanzibar na Familia yake baada ya kuapicha leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akiwa na Mkewe na Watoto wake katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa Ikulu Zanzibar leo.


Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Nd,Ibrahim Mzee na Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar George Kazi ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis na Mstahiki Meya wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib ni miongoni mwa  Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said akiwa katika ukumbi wa mikutamo  Ikulu Mjini Unguja na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mshibe Ali Bakari   kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

 Viongozi mbali mbali na watendaji waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,(Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,(Picha na Ikulu.]
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                                                  26.3.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha  Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika wadhifa huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa  chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Miongoni mwao ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis.

Wengine ni  Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh  Mahmoud Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

No comments :

Post a Comment